Luka MT. 23
23
1WAKAONDOKA jamii yote, wakamleta kwa Pilato. 2Wakaanza kumshitaki, wakisema, Tumemwona mtu huyu amipotosha taifa letu, anawakataza watu wasimpe Kaisari kodi, akisema ya kwamba yeye mwenyewe yu Kristo, mfalme. 3Pilato akamwuliza, akisema, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Akajibu, akamwambia, Unasema wewe. 4Pilato akawaambia makuhani wakuu na makutano, Mimi sioni khatiya yo yote katika mtu huyu. 5Nao wakamshurutisha, wakisema, Awataharakisha watu, akifundisha katika Yahudi yote, akianzia Galilaya hatta hapa. 6Pilato aliposikia neno hili Galilaya, akauliza, Mtu huyu ni Mgalilaya? 7Alipojua ni chini ya mamlaka ya Herode, akampeleka kwa Herode; nae alikuwa katika Yerusalemi siku zile. 8Na Herode alipomwona Yesu, akafurahiwa sana: kwa kuwa tangu zamani alikuwa akitaka kumwona, kwa sababu amesikia mambo yake; akataraja kuona ishara inafanyika nae. 9Akamwuliza kwa maneno mengi, yeye asimjibu lo lote. 10Wakasimama makuliani wakuu na waandishi, wakimshitaki kwa nguvu. 11Bassi Herode akamtweza pamoja na askari zake akamdhihaki, akamvika mavazi mazurimazuri, akamrudisha kwa Pilato. 12Ndipo Herode na Pilato wakapatana, siku ileile; kwa maana kwanza walikuwa na uadui wao kwa wao. 13Pilato akawaita pamoja makuhani wakuu, na wakubwa, na watu, akawaambia, 14Mmeniletea mtu huyu, kana kwamba anapotosha watu; nami hassi nilipomhukumu mbele yenu, sikuona khatiya katika mtu huyu katika yale mliyomshitaki; 15wala Herode nae; kwa maana naliwapelekeni kwake, wala hapana neno la kustahili kufa lililotendwa nae.
16Bassi nikiisha kumrudi, nitamfungua. 17Maana ilimlazimu kuwafungulia mmoja wakati wa siku kuu. 18Wakapiga kelele wote pamoja, wakisema, Mchukue huyu, tufungulie Barabba. 19Nae ni mtu aliyetiwa gerezani kwa sababu ya fitina iliyofanyika mjini, na kwa uuaji. 20Bassi marra ya pili Pilato akasema nao, akitaka kumfungua Yesu. 21Nao wakalia, wakisema, Msulibishe, msulibishe. 22Nae akawaambia marra ya tatu, Kwani? ubaya gani alioutenda huyu? sikuona hatta neno kwake la kustahili kufa; bassi nikiisha kumrudi nitamfungua. 23Lakini wakakaza kusema kwa santi kuu, wakitaka asulibiwe; zikashinda sauti zao na za makuhani wakuu. 24Pilato akakata maneno yafanyike waliyoyataka. 25Akamfungua yeye aliyetiwa gerezani kwa fitina na uuaji, waliyemtaka: akatoa Yesu kwa mapenzi yao. 26Walipokuwa wakimchukua, wakamshika Mkurene Simon, aliyekuwa akitoka shamba, wakamtwika yeye msalaba, auchukue nyuma yake Yesu. 27Wakamfuata makutano mengi ya watu, na ya wanawake, waliojipigapiga, wakaomboleza. 28Yesu akawageukia, akasema, Binti za Yerusalemi, msinililie mimi, bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu. 29Kwa maana siku zinakuja watakaposema, Wa kheri walio tassa, na matumbo yasiyozaa, na maziwa yasiyonyonyesha. 30Ndipo watakapoanza kuiambia milima, Tuangukieni, na vilima, Tusetirini. 31Kwa kuwa wakifanya haya wakati wa mti ulio mbichi, wakati wa ule ulio mkavu yatakuwaje? 32Wakachukuliwa wawili tena, wakhalifu, wauawe pamoja nae. 33Hatta walipofika pahali paitwapo Kichwa, ndiko walikomsulibisha, na wale wakhalifu, mmoja mkono wa kuume, na mmoja mkono wa kushoto. 34Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui watendalo. Wakagawanya nguo zake, wakipiga kura. 35Watu wakasimama, wakitazama. Nao wakuu wakamfanyizia mzaha, wakisema, Aliokoa wengine; na ajiokoe nafsi yake, kama huyu ndiye Kristo wa Mungu, mtenle wake. 36Askari wakamdhihaki, wakimjia, wakimpa siki, na kusema, 37Kama wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi, njiokoe nafsi yako. 38Palikuwa na anwani juu yake kwa harufi za kiyunani na kirumi na kiebrania, HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI. 39Mmoja wa wale wakhalifu waliotundikwa akamtukana, akisema, Si wewe uliye Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi. 40Wa pili akajibu, akamkemea akasema, Humwogopi wewe hatta Mungu, ukiwa katika hukumu ile ile? 41Na sisi kweli ina haki; kwa maana sisi tunalipwa ijara ya haki ya matendo yetu: bali huyu hakutenda neno lisilofaa. 42Akamwambia Yesu, Bwana, unikumbuke ujapo katika ufalme wako. 43Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo utakuwa pamoja nami Peponi. 44Ikapata kama saa a sita, pakawa giza juu ya inchi yote hatta saa a tissa, 45jua likipunguka: pazia ya hekalu ikapasuka katikati. 46Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu: na alipokwisha kusema haya akatoa roho. 47Akida alipoona lililokuwa, akamtukuza Mungu, akisema, Kwa kweli mtu huyu alikuwa mwenye haki. 48Na makutano wote waliokusanyika kutazama haya, walipotazama yaliyofanyika, wakarudi, wakijipiga vifua. 49Marafiki zake wote wakasimama kwa mbali, nao wanawake waliofuatana nae toka Galilaya, wakiangalia haya, 50Akatoka mtu, jina lake Yusuf, nae ni mtu wa baraza yao, mtu mwema, mwenye haki 51(mtu huyu hakuwa akikubali shauri lao wala tendo lao), mwenyeji wa Arimathaya, mji wa Wayahudi, nae mwenyewe akiutazamia ufalme wa Mungu. 52Bassi mtu huyu akamwendea Pilato akaomba apewe mwili wa Yesu. 53Akaushusha, akauzinga nguo za katani, akauweka katika kaburi lililochongwa mwambani; hajawekwa mtu aliye yote ndani yake kamwe. 54Ilikuwa siku ya Maandalio, sabato ikawadia. 55Wanawake wakafuatana nao, wale waliokuja pamoja nae kutoka Galilaya, wakalitazama kaburi na jinsi ulivyowekwa mwili wake. Wakarudi wakafanya tayari manukato na marhamu. 56Na siku ya sabato wakastarehe kama ilivyoamriwa.
Селектирано:
Luka MT. 23: SWZZB1921
Нагласи
Сподели
Копирај
Дали сакаш да ги зачуваш Нагласувањата на сите твои уреди? Пријави се или најави се
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.