Mwanzo 15
15
Agano la Mungu na Abramu
1Baada ya mambo hayo, neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Abramu katika maono, “Abramu! Usiogope! Mimi ni ngao yako.#15:1 Mimi ni ngao yako: Yaani, Mungu ndiye mlinzi au kinga yake. Taz Zab 3:3 maelezo. Tuzo lako litakuwa kubwa!” 2Lakini Abramu akasema, “Ee Mwenyezi-Mungu, utanipa nini hali naendelea kuishi bila mtoto, na mrithi wangu ni Eliezeri wa Damasko? 3Tazama! Hujanijalia mtoto; mtumwa aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye atakayekuwa mrithi wangu!”#15:2-3 Lalamiko la Abrahamu kwamba hana mtoto atakayemrithi, linafuatiwa na jibu la Mungu ambaye anathibitisha ahadi yake (aya ya 5) na kufanya agano naye (aya ya 18). Taz Mwa 12:2 maelezo.
4Ndipo Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Huyu hatakuwa mrithi wako! Mwanao halisi ndiye atakayekuwa mrithi wako.” 5Hapo Mwenyezi-Mungu akamleta Abramu nje na kumwambia, “Tazama mbinguni! Zihesabu nyota, kama kweli utaweza kuzihesabu! Hivyo ndivyo wazawa wako watakavyokuwa wengi!” 6Abramu akamwamini Mwenyezi-Mungu,#15:6 Abramu akamwamini Mwenyezi-Mungu: Imani ya Abahamu ilikuwa kitendo chake binafsi cha kujiweka mikononi mwa Mungu na kuamini ahadi yake (Rom 4:3,9,22; Gal 3:6: Yak 2:23). “Naye Mwenyezi-Mungu akamkubali Abramu kuwa mwadilifu”: Uadilifu ambao Mungu alimjalia Abrahamu unategemea imani yake. Kwa hiyo, Paulo anapoongea juu ya imani ambayo ni muhimu katika kupata wokovu anamchukua Abrahamu kama mfano (Rom 3:6-22). naye Mwenyezi-Mungu akamkubali Abramu kuwa mwadilifu.
7Mwenyezi-Mungu akamwambia Abramu, “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu niliyekuleta toka Uri, mji wa Wakaldayo, ili nikupe nchi hii uimiliki.” 8Lakini Abramu akamwambia, “Ee Mwenyezi-Mungu, nitajuaje kwamba nitaimiliki nchi hii?” 9Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Niletee ndama wa miaka mitatu, mwanambuzi jike wa miaka mitatu, kondoo dume wa miaka mitatu, na hua na kinda la njiwa.”#15:9 Niletee ndama …mwanambuzi … kondoo … hua … njiwa: Hawa wanyama ni vitu vilivyotakiwa hapo kale kwa kuadhimisha agano au mkataba au mma. Wanyama walikatwa sehemu mbili (aya 10) na watu waliohusika katika mma huo au agano walipita katikati ya hizo nusu za kafara wakitamka kiapo na kulaani yeyote atakayekiuka agano hilo. Kitendo cha kuwakata nusu hao wanyama kilikuwa pia kitendo cha ishara au mfano, yaani atakayevunja agano hilo atapatwa na hali hiyo ya hao wanyama. Rejea Yer 34:18-19. 10Abramu akamletea hao wote, akamkata kila mnyama vipande viwili, akavipanga katika safu mbili, vikielekeana; lakini ndege hakuwakata vipande viwili. 11Na tai walipoijia hiyo mizoga, Abramu akawa anawafukuza.
12Jua lilipokuwa likitua, Abramu alishikwa na usingizi mzito;#15:12 Abramu alishikwa na usingizi mzito: Huu usingizi mzito unatukumbusha ule usingizi mzito wa Adamu (Mwa 2:21). Kiebrania katika sehemu hizi mbili kinatumia neno lile lile. Rejea pia Yobu 4:13. hofu na giza nene vikamfunika. 13Hapo Mwenyezi-Mungu akamwambia Abramu, “Ujue hakika ya kwamba wazawa wako watakaa kama wageni katika nchi isiyo yao, watakuwa watumwa na watateswa kwa muda wa miaka 400.#15:13 Dokezo kwa utumwa wa Waisraeli kule Misri. Rejea Kut 1:1-14; 12:40-41; Mate 7:6. 14Hata hivyo, nitaliadhibu taifa watakalolitumikia, na hatimaye watatoka wakiwa na mali nyingi. 15Lakini wewe mwenyewe utaishi maisha marefu na kufariki kwa amani. 16Wazawa wako watarudi hapa katika kizazi cha nne, kwa sababu uovu wa Waamori haujakamilika bado.”#15:16 Waamori: Hapa, jina hili linataja jumla ya watu wa kale wa Kanaani kabla ya watu wa Israeli kuhamia huko. Na kuhusu huo “uovu wa Waamori” rejea Kut 23:23-24; 34:11-16.
17Jua lilipokwisha tua na giza kuingia, tanuri ifukayo moshi na mwenge uwakao moto#15:17 Tanuri ifukayo moshi na mwenge uwakao moto: Mafungu haya mawili ya maneno yanatumiwa katika Biblia kuashiria kuweko kwake Mungu. vikapita katikati ya vile vipande vya nyama. 18Siku hiyo, Mwenyezi-Mungu akafanya agano na Abramu akisema, “Wazawa wako ninawapa nchi hii, toka mto wa Misri#15:18 Mto wa Misri: Wengi wanafikiri hapa haihusu Mto Nili bali kijito kingine cha Misri (Yos 15:4) kusini mashariki ya Palestina karibu na pwani ya Mediteranea. Na kuhusu “Mto Eufrate”, taz Mwa 2:10-14 maelezo. hadi ule mto mkubwa wa Eufrate, 19yaani nchi za Wakeni, Wakenizi, Wakadmoni, 20Wahiti, Waperizi, Warefai, 21Waamori, Wakanaani, Wagirgashi na Wayebusi.”#15:19-21 Orodha hii inataja watu wa Palestina kabla ya watu wa Israeli kuwasili huko. Orodha hii karibu inafanana na zile za Kut 13:5; 23:23,28; 33:2; 34:11; 38:17; Kumb 7:1; 20:17; Yos 3:10.
Одоогоор Сонгогдсон:
Mwanzo 15: BHNTLK
Тодруулга
Хуваалцах
Хувилах
Тодруулсан зүйлсээ бүх төхөөрөмждөө хадгалмаар байна уу? Бүртгүүлэх эсвэл нэвтэрнэ үү
Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993
The Bible Society of Kenya 1993