Mwanzo UTANGULIZI
UTANGULIZI
Kitabu cha Mwanzo ndicho cha kwanza katika orodha ya vitabu vya Biblia. Jina Mwanzo linatokana na kitabu chenyewe (1:1) kwa maana ya asili na chanzo cha ulimwengu, mtu, dhambi, kifo na taifa la Israeli. Jambo la msingi ni Mungu na mtu katika uhusiano wao na pia mpango wa Mungu wa wokovu na uteule wa watu wa wake.
Mungu ndiye Muumba wa vitu vyote. Mungu alimwumba mtu, lakini mtu huyo alimwasi Muumba wake, na kwa uasi wake watu wote wakawa wenye dhambi. Matokeo ya dhambi yakawa kifo. Kwa kuwa tangu mwanzo Mungu aliahidi kuujalia uumbaji wake baraka zake. Ndipo hata mtu alipoasi, Mungu aliendelea kujifunua kwake, kunena na wateule wake, kuwapa wajibu na kuwabariki.
Yaliyomo:
1. Simulizi la awali kuhusu ulimwengu na mtu, Sura 1—11
(a) Kuumba ulimwengu (1—2)
(b) Uasi na kuanguka kwa mtu (3)
(c) Uasi unaongezeka (4—5)
(c) Nuhu na gharika (6—9)
(d) Mnara wa Babeli (10—11)
2. Historia ya awali ya Waisraeli, Sura 12—50
(a) Habari za Abrahamu na watoto wake (12—24)
(b) Habari za Yakobo (25—36)
(c) Habari za Yusufu (37—50)
Terpilih Sekarang Ini:
Mwanzo UTANGULIZI: SRUVDC
Highlight
Kongsi
Salin
Ingin menyimpan sorotan merentas semua peranti anda? Mendaftar atau log masuk
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.