Yohana Utangulizi

Utangulizi
Miongoni mwa Injili zote nne, Injili ya Yohana ni ya kipekee. Ingawa kwa ujumla inaonesha maisha ya Isa na huduma yake, Injili hii haina mifano. Injili ya Yohana inaelezea miujiza saba; kuna miwili iliyonakiliwa katika Injili zile zingine, na miujiza mitano ambayo Yohana peke yake aliielezea.
Yohana anaandika jinsi Isa anavyojidhihirisha kuwa ni Mwenyezi Mungu kwa semi saba za “Mimi Ndiye”. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu alivyojidhihirisha kwa Waisraeli huko Misri. Kwa hiyo, ni wazi kwamba Isa ni Yehova.
Mwandishi
Yohana mwana wa Zebedayo, nduguye Yakobo.
Kusudi
“Lakini haya yameandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Isa ndiye Al-Masihi, Mwana wa Mwenyezi Mungu, na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake” (20:31).
Mahali
Uwezekano mkubwa ni kwamba Injili hii iliandikiwa Efeso.
Tarehe
Mnamo 85–90 B.K.
Wahusika Wakuu
Isa, mama yake, na wanafunzi wake Isa; Yahya na wanafunzi wake; Mariamu, Martha na Lazaro; Pilato, wakuu wa dini ya Kiyahudi, na Mariamu Magdalene.
Wazo Kuu
Injili ya Yohana inatilia mkazo zaidi Uungu wa Al-Masihi. Pia inatueleza kwa undani zaidi ishara ambazo Injili zingine zinaziita miujiza, ili msomaji aweze kuamini kwamba Isa ndiye Al-Masihi, Mwana wa Mwenyezi Mungu, na kwamba mtu anaweza kupata uzima wa milele tu kwa kumwamini Isa.
Mambo Muhimu
Katika Injili hii, tunapata habari kuhusu baadhi ya miujiza ya Isa, na mafundisho yake ambayo hayakutajwa katika Injili zingine. Sehemu ya sura 14–17 inaeleza kwa kina mafundisho ambayo Isa aliwapa wanafunzi wake kabla ya kifo chake. Sehemu ya mwisho inafafanua jinsi Isa alivyojidhihirisha kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka kwake.
Yaliyomo
Neno alifanyika mwili (1:1-18)
Huduma ya Isa kabla ya kurudi Galilaya (1:19–4:54)
Huduma ya Isa huko Galilaya, na upinzani uliomkabili huko Yerusalemu (5:1–10:42)
Isa amfufua Lazaro (11:1-57)
Isa akamilisha huduma yake (12:1–13:30)
Mafundisho ya mwisho ya Bwana Isa (13:31–17:26)
Kufa na kufufuka kwa Isa (18:1–20:10)
Isa aonekana baada ya kufufuka (20:11–21:25).

Выделить

Поделиться

Копировать

None

Хотите, чтобы то, что вы выделили, сохранялось на всех ваших устройствах? Зарегистрируйтесь или авторизуйтесь