Mufananidzo weYouVersion
Mucherechedzo Wekutsvaka

Yohana 16

16
1“Nimewaambia mambo haya yote ili msije mkaiacha imani. 2Watawatenga na masinagogi#16:2 Nyumba za ibada na mafunzo.. Naam, saa yaja ambayo mtu yeyote atakayewaua atadhani kwa kufanya hivyo anamtumikia Mungu. 3Nao watawatenda haya kwa sababu hawamjui Baba wala mimi. 4Lakini nimewaambia ninyi mambo haya, ili saa hiyo ikiwadia mpate kukumbuka ya kuwa nilikuwa nimewaambia. Sikuwaambia mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi.
5“Sasa mimi ninaenda kwake yeye aliyenituma, lakini hakuna hata aniulizaye, ‘Unaenda wapi?’ 6Kwa sababu nimewaambia mambo haya, mioyo yenu imejawa na huzuni. 7Lakini nawaambia kweli, yafaa mimi niondoke, kwa kuwa nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; lakini nikienda nitamtuma kwenu. 8Naye atakapokuja, atauthibitishia ulimwengu kuhusu dhambi, haki na hukumu. 9Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi; 10kwa habari ya haki, kwa sababu ninaenda kwa Baba, nanyi hamtaniona tena; 11kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.
12“Bado ninayo mambo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili sasa. 13Atakapokuja huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie katika kweli yote. Yeye hatanena kwa ajili yake mwenyewe, bali atanena yale yote atakayosikia, naye atawaonesha mambo yajayo. 14Atanitukuza mimi, kwa maana atayachukua yaliyo yangu na kuwajulisha ninyi. 15Vyote alivyo navyo Baba ni vyangu. Ndiyo maana nimesema Roho atachukua yaliyo yangu na kuwajulisha ninyi.”
Huzuni itageuka kuwa furaha
16Isa akaendelea kusema, “Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona.”
17Baadhi ya wanafunzi wakaulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona’? Naye ana maana gani asemapo, ‘Kwa sababu ninaenda kwa Baba’?” 18Wakaendelea kuulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘Kitambo kidogo’? Hatuelewi hilo analosema.”
19Isa akatambua kuwa walitaka kumuuliza kuhusu hilo, hivyo akawaambia, “Je, mnaulizana nina maana gani niliposema, ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona’? 20Amin, amin nawaambia, ninyi mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utafurahi. Ninyi mtahuzunika, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. 21Mwanamke anapokuwa na uchungu wa kuzaa huwa na maumivu kwa sababu saa yake imewadia. Lakini baada ya mtoto kuzaliwa, yule mwanamke husahau maumivu hayo kwa sababu ya furaha yake ya kuzaliwa mtoto ulimwenguni. 22Hivyo ninyi mna maumivu sasa, lakini nitawaona tena, nayo mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye. 23Katika siku hiyo hamtaniuliza neno lolote. Amin, amin nawaambia, mkimwomba Baba jambo lolote kwa jina langu, yeye atawapa. 24Hadi sasa hamjaomba jambo lolote kwa Jina langu. Ombeni nanyi mtapewa, ili furaha yenu ipate kuwa kamili.
Amani kwa wanafunzi
25“Nimewaambia mambo haya kwa mafumbo. Saa yaja ambapo sitazungumza nanyi tena kwa mafumbo bali nitawaeleza waziwazi kuhusu Baba. 26Siku hiyo mtaomba kwa Jina langu. Wala sitawaambia kwamba nitamwomba Baba kwa ajili yenu, 27kwa maana Baba mwenyewe anawapenda, kwa sababu mmenipenda mimi na mmeamini kwamba nimetoka kwa Mungu. 28Nilitoka kwa Baba na kuja ulimwenguni; sasa naondoka ulimwenguni na kurudi kwa Baba.”
29Ndipo wanafunzi wake wakasema, “Sasa unazungumza waziwazi, wala si kwa mafumbo. 30Sasa tumejua kwamba wewe unajua mambo yote, wala hakuna haja ya mtu kukuuliza maswali. Kwa jambo hili tunaamini kwamba ulitoka kwa Mungu.”
31Isa akawajibu, “Je, sasa mnaamini? 32Saa inakuja, naam, imekwisha kuwadia, mtakapotawanyika kila mmoja kwenda nyumbani mwake na kuniacha peke yangu. Lakini mimi siko peke yangu kwa sababu Baba yu pamoja nami.
33“Nimewaambia mambo haya ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki. Lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu.”

Zvasarudzwa nguva ino

Yohana 16: NENO

Sarudza vhesi

Pakurirana nevamwe

Sarudza zvinyorwa izvi

None

Unoda kuti zviratidziro zvako zvichengetedzwe pamidziyo yako yose? Nyoresa kana kuti pinda