1 Mose 5
5
Vizazi vya Adamu.
(Taz. 1 Mambo 1:1-4.)
1Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku hiyo Mungu alipomwumba mtu alimtengeneza kwa mfano wake Mungu;#1 Mose 1:27; Luk. 3:38. 2akamwumba kuwa mume na mke, akawabariki, akawaita jina lao Adamu (Mtu) siku hiyo, walipoumbwa. 3Adamu alikuwa mwenye miaka 130 alipozaa mwana aliyefanana naye kwa kuwa mfano wake, akamwita jina lake Seti. 4Alipokwisha kumzaa Seti, siku zake Adamu zikawa tena miaka 800, akazaa wana wa kiume na wa kike. 5Siku zake Adamu, alizokuwapo, zote zikawa miaka 930, kisha akafa.
6Seti alikuwa mwenye miaka 105 alipomzaa Enosi. 7Alipokwisha kumzaa Enosi Seti akawapo miaka 807, akazaa wana wa kiume na wa kike. 8Siku zake Seti zote zikawa miaka 912, kisha akafa.
9Enosi alikuwa mwenye miaka 90 alipomzaa Kenani. 10Alipokwisha kumzaa Kenani Enosi akawapo miaka 815, akazaa wana wa kiume na wa kike. 11Siku zake Enosi zote zikawa miaka 905, kisha akafa.
12Kenani alikuwa mwenye miaka 70 alimpomzaa Mahalaleli. 13Alipokwisha kwisha kumzaa Mahalaleli, Kenani akawapo miaka 840, akazaa wana wa kiume na wa kike. 14Siku zake Kenani zote zikawa miaka 910, kisha akafa.
15Mahalaleli alikuwa mwenye miaka 65 alipomzaa Yaredi. 16Alipokwisha kumzaa Yaredi Mahalaleli akawapo miaka 830, akazaa wana wa kiume na wa kike. 17Siku zake Mahalaleli zote zikawa miaka 895, kisha akafa.
18Yaredi alikuwa mwenye miaka 162 alipomzaa Henoki. 19Alipokwisha kumzaa Henoki Yaredi akawapo miaka 800, akazaa wana wa kiume na wa kike. 20Siku zake Yaredi zote zikawa miaka 962, kisha akafa.
21Henoki alikuwa mwenye miaka 65 alipomzaa Metusela.#1 Mose 6:9; Yuda 14. 22Naye Henoki alifanya mwenendo wa kushikana na Mungu alipokwisha kumzaa Metusela akawapo miaka 300, akazaa wana wa kiume na wa kike. 23Siku zake Henoki zote zikawa miaka 365.#Ebr. 11:5; 2 Fal. 2:11; Yes. 57:1-2. 24Kwa kuwa Henoki alifanya mwenendo wa kushikana na Mungu, mara akawa hayuko tena, kwani Mungu alimchukua.
25Metusela alikuwa mwenye miaka 187 alipomzaa lameki. 26Alipokwisha kumzaa Lameki akawapo miaka 782, akazaa wana wa kiume na wa kike. 27Siku zake Metusela zote zikawa miaka 969, kisha akafa. 28Lameki alikuwa mwenye miaka 182 alipozaa mwana.#1 Mose 3:17-19. 29Akamwita jinala lake Noa (Tulia) kwa kwamba: Huyu ndiye atakayetutuliza mioyo kwa ajili ya kazi zetu, mikono yetu inazozifanya kwa uchungu katika nchi, aliyoiapiza Bwana. 30Alipokwisha kumzaa Noa Lameki akawapo miaka 595, akazaa wana wa kiume na wa kike. 31Siku zake Lameki zote zikawa miaka 777, kisha akafa. 32Noa alikuwa mwenye miaka 500 alipozaa wana; Semu, Hamu na Yafeti.
Trenutno izabrano:
1 Mose 5: SRB37
Istaknuto
Podijeli
Kopiraj
Želiš li da tvoje istaknuto bude sačuvano na svim tvojim uređajima? Kreiraj nalog ili se prijavi
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.