1 Mose 6
6
Ubaya wa watu.
1Watu walipoanza kuwa wengi katika nchi, nao wna wa kike walipozaliwa kwao,#Mat. 24:38. 2nao wana wa Mungu walipowaona wana wa kike wa watu kuwa wazuri, wakajichukulia wake kwao wote, waliowachagua. 3Ndipo, Bwana aliposema: Roho yangu haiwezi kubishana na watu kale na kale, kwani kwa hivyo, walivyopotea, mioyo yao imegeuka kuwa nyama tupu. Basi, siku zao na ziwe bado miaka 120. 4Siku zile walikuwako katika nchi nao watu walio majitu; hata baadaye siku zote wana wa Mungu walipoingia kwao wana wa kike na watu, nao waliwazalia wana; hawa ndio wale wenye nguvu waliojipatia jina kuu tangu kale.
5Bwana alipoona, ya kuwa ubaya wa watu ni mwingi katika nchi, nayo yote, waliyoyalinganya na kuyawaza mioyoni mwao, ni mabaya tu siku zote,#1 Mose 8:21. 6ndipo, Bwana alipojuta, akaumizwa sana moyoni mwake, ya kuwa aliwafanya watu wa kukaa katika nchi.#4 Mose 23:19; Sh. 18:27; Yer. 18:10. 7Kwa hiyo Bwana akasema: Nitawafuta watu, niliowaumba, watoweke katika nchi, wao watu nao nyama na wadudu na ndege wa angani, kwani ninajuta, ya kuwa niliwafanya.
Noa.
8Noa akapata upendeleo machoni pake Bwana. 9Hivi ndivyo vizazi vyake Noa: Noa alikuwa mtu mwongofu mwenye kumcha Mungu miongoni mwao, aliozaliwa nao, kwani Noa alifanya mwenendo wa kushikana na Mungu.#Ebr. 11:7; 1 Mose 5:22,24. 10Noa akazaa wana watatu: Semu, Hamu na Yafeti. 11Nayo nchi ilikuwa imegeuka kuwa mbaya machoni pake Mungu, hiyo nchi ikijaa ukorofi. 12Mungu alipoitazama nchi akaiona kuwa mbaya, kwani wote wenye miili walishika njia mbaya katika nchi.#Sh. 14:2-3.
Mungu anamfumbulia Noa atakayoyafanya.
13Ndipo, Mungu alipomwambia Noa: Mwisho wao wote wenye miili umefika machoni pangu, kwani wameijaza nchi makorofi yao, kwa hiyo wataniona, nikiwaangamiza pamoja na nchi.#Amo. 8:2. 14Jitengenezee chombo kikubwa sana cha miti ya mivinje! Humo chomboni ndani ukate vyumba! Kisha kipake lami upande wa ndani nao wa nje! 15Navyo ndivyo, utakavyokitengeneza: urefu wa hicho chombo uwe mikono 30, nao upana wake mikono 50, nao urefu wake wa kwenda juu mikono 300. 16Juu yake hicho chombo utengeneze mahali pa kuingizia mwanga, upana wake uwe mkono mmoja; napo upafanye, pazunguke huko juu, nao mlango wa chombo uweke mbavuni pake! Utengeneze nayo madari matatu, la chini, la kati, la juu! 17Kwani tazama: Mimi nitaleta mafuriko ya maji juu ya nchi, niwaangamize wote wenye miili walio na pumzi za uzima, walioko chini ya mbingu; wote pia wanaokaa katika nchi sharti wafe. 18Lakini wewe nitakuwekea agano: Utaingia mle chomboni, wewe na wanao na mkeo nao wake wa wanao pamoja na wewe. 19Tena miongoni mwao nyama wote wenye miili utaingiza mle chomboni wawili wawili, wa kiume na wa kike, niwaponye pamoja na wewe, 20nao ndege wa kila namna nao nyama wa nyumbani wa kila namna, nao wadudu wote wa nchi wa kila namna; wao wote na waingie kwako wawili wawili, niwaponye. 21Kisha wewe jichukulie vilaji vyote vinavyoliwa, uvikusanye kwako, viwe chakula chako wewe nacho chao. 22Nao akayafanya yote; kama Mungu alivyomwagiza, ndivyo, alivyoyafanya.
Trenutno izabrano:
1 Mose 6: SRB37
Istaknuto
Podijeli
Kopiraj
Želiš li da tvoje istaknuto bude sačuvano na svim tvojim uređajima? Kreiraj nalog ili se prijavi
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.