Luka 19
19
Zakeo.
1*Alipoingia Yeriko akapita kati ya mji. 2Mle akaona mtu aliyeitwa jina lake Zakeo, alikuwa mkubwa wa watoza kodi, tena mwenye mali. 3Alitaka kumwona Yesu, alivyo, lakini hakuweza, kwa sababu watu walikuwa wengi, naye alikuwa mfupi kwa umbo lake. 4Akapiga mbio, aje mbele, akapanda mtamba, apate kumwona, kwani njia yake ilipitia papo hapo. 5Yesu alipofika hapo akatazama juu, akamwambia: Zakeo, shuka upesi! Kwani leo sharti nikae nyumbani mwako! 6Ndipo, aliposhuka upesi, akampokea na kufurahi. 7Lakini walioviona wakamnung'unikia wote wakisema: Ameingia nyumbani mwake mkosaji na kutua humo.#Luk. 15:2. 8Zakeo akainuka, akamwambia Bwana: Tazama, Bwana, nusu yao vyote, nilivyo navyo, nawapa maskini, tena kama nimepunja mtu, namrudishia mara nne.#2 Mose 22:1; Ez. 33:14-15. 9Lakini Yesu akamwambia: Leo nyumbani humu mmeonekana wokovu, kwani mwenyewe naye ni mwana wa Aburahamu.#Luk. 13:16; Mat. 10:6. 10Kwani Mwana wa mtu amejia kutafuta na kuokoa kilichopotea.*#Luk. 5:32; 1 Tim. 1:15.
Watumwa wa mfalme.
(11-27: Mat. 25:14-30.)
11*Watu walipoyasikia hayo, akaongeza kusema na kutoa mfano. Kwa sababu alikuwa karibu ya Yerusalemu, watu wakawaza kwamba: Ufalme wa Mungu sharti utokee sasa hivi. 12Kwa hiyo akasema: Mtu wa kifalme alikwenda kufika katika nchi ya mbali, ajipatie ufalme, kisha arudi.#Mar. 13:34. 13Akawaita watumwa wake kumi, akawapa mia kumi za shilingi, akawaambia: Zichuuzieni, mpaka nitakaporudi! 14Lakini wenyeji wake walimchukia, wakatuma wajumbe nyuma yake wakisema: Hatumtaki huyu, atutawale sisi.#Yoh. 1:11. 15Ikawa, alipokwisha kuupata ule ufalme, akarudi akaagiza, waitwe wale watumwa, aliowapa fedha, waje kwake, apate kujua, kila mtu alivyojipatia kwa kuzichuuzia. 16Alipokuja wa kwanza, akasema: Bwana, shilingi zako mia zimeleta mia kumi nyingine. 17Naye akamwambia: Vema, wewe mtumwa mwema, ulikuwa mwelekevu wa machache, utatwaa miji kumi, uitawale!#Luk. 16:10. 18Alipokuja wa pili, akasema: Bwana, shilingi zako mia zimeleta mia tano. 19Huyu naye akamwambia: Wewe nawe twaa miji mitano, uitawale! 20Alipokuja mwingine wao akasema: Bwana, tazama hapa shilingi zako mia! Nimekuwa nimeziweka katika mharuma. 21Kwani nilikuogopa, kwa kuwa wewe u mkorofi, hutwaa usiyoyaweka, huvuna usioyoyapanda. 22Akamwambia: Kwa maneno yako wewe ninakuumbua, wewe mtumwa mbaya! Ulinijua, ya kuwa mimi ni mkorofi, hutwaa nisiyoyaweka, huvuna nisiyoyapanda? 23Basi, kwa nini hukumpa mwenye duka fedha zangu? Nami nilipokuja ningalizichukua pamoja na faida? 24Akawaambia walioko: Zichukueni shilingi zake mia, mmpe yule mwenye mia kumi! 25Wakamwambia: Bwana, anazo mia kumi! 26(Akajibu:) Nawaambiani: Kila mwenye mali atapewa; lakini asiye na kitu, atachukuliwa hata kile, alicho nacho.#Luk. 8:18; Mat. 13:12. 27Lakini wale wachukivu wangu wasionitaka, niwatawale, mwalete hapa, mwachinje mbele yangu!*
Kuingia Yerusalemu.
(29-38: Mat. 21:1-9; Mar. 11:1-10; Yoh. 12:12-16.)
28Alipokwisha kuyasema hayo akaendelea kusafiri, akapanda kwenda Yerusalemu. 29Ikawa, alipokaribia Beti-Fage na Betania penye mlima unaoitwa Wa Michekele, akatuma wanafunzi wawili 30akisem: Nendeni katika kijiji kinachowaelekea! Mtakapoingia mle mtaona, pamefungwa mwana punda, ambaye mtu hajampanda bado; mfungueni, mmlete! 31Kama mtu atawauliza: Mbona mnamfungua? semeni hivi: Bwana wetu anamtakia kazi! 32Wao waliotumwa walipoondoka kwenda wakaviona, kama alivyowaambia. 33Walipomfungua mwana punda, wenyewe wakawauliza: Kwa sababu gani mnamfungua mwana punda? 34Nao wakasema: Bwana anamtakia kazi. 35Kisha wakampeleka kwa Yesu, wakatandika nguo zao upesiupesi juu ya mwana punda, wakampandisha Yesu. 36Alipokwenda, wakatandika nguo zao njiani. 37Alipofika kwenye mtelemko wa mlima wa michekele, wingi wote wa wanafunzi ukaanza kushangilia na kumsifu Mungu wakipaza sauti kwa ajili ya matendo yote ya nguvu, waliyoyaona. 38Wakasema:
Na atukuzwe ajaye kuwa mfalme kwa Jina la Bwana!
Mbinguni uko utengemano,
nao utukufu uko juu mbinguni!#Luk. 2:14. 39Hapo palikuwa na Mafariseo mle kundini mwa watu, wakamwambia: Mfunzi, wakaripie wanafunzi wako! 40Akajibu akisema: Nawaambiani:
Hawa watakaponyamaza, mawe yatapiga makelele.#Hab. 2:11.
Kuulilia mji.
41*Alipofika karibu, akautazama ule mji, akaulilia akisema:#2 Fal. 8:1; Yoh. 11:35. 42Ungaliyatambua na wewe siku hii ya leo yanayokupa utengemano! Lakini sasa yamefichika, macho yako yasiyaone!#5 Mose 32:29. 43Kwani siku zitakujia, adui zako watakapokujengea boma, likuzinge, wapate kukuhangisha po pote. 44Nao watakubomolea wewe na watoto wako waliomo mwako, wasiache mwako jiwe, lishikane na jiwe lenziwe, kwa sababu hukuzitambua siku, ulipokaguliwa.#Luk. 21:6.
Kuwafukuza wachuuzi Patakatifu.
(45-48: Mat. 21:12-16; Mar. 11:15-18; Yoh. 2:13-16.)
45Akapaingia Patakatifu, akaanza kuwafukuza wenye kuchuuzia pale, 46akawaambia: Imeandikwa: Nyumba yangu sharti iwe nyumba ya kuombea, lakini ninyi mmeigeuza kuwa pango la wanyang'anyi.#Yes. 56:7; Yer. 7:11. 47Kisha akawa akifundishia Patakatifu kila siku. Lakini watambikaji wakuu na waandishi na wakubwa wa watu wakatafuta kumwangamiza, 48wasione njia ya kuyafanya; kwani watu wote pia walishikamana naye na kumsikiliza.*
Trenutno izabrano:
Luka 19: SRB37
Istaknuto
Podijeli
Kopiraj
Želiš li da tvoje istaknuto bude sačuvano na svim tvojim uređajima? Kreiraj nalog ili se prijavi
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.