Luka 23
23
Yesu mbele ya Pilato.
(1-25: Mat. 27:2,11-31; Mar. 15:1-20; Yoh. 18:28-19:16.)
1Kisha wakainuka wale watu wengi wote pia, wakampeleka kwa Pilato. 2Wakaanza kumsuta wakisema: Huyu tulimwona, anavyowapindua watu wa taifa letu na kuwakataza, wasitoe kodi za Kaisari, akisema: Mimi Kristo ni mfalme.#Luk. 20:25. 3Pilato alipomwuliza akisema: Wewe ndiwe mfalme wa Wayuda? akamjibu akisema: Wewe unavyosema, ndivyo. 4Pilato akawaambia watambikaji wakuu na makundi ya watu kwake huyu mtu sioni neno la kumhukumu. 5Lakini wale wakakaza sana kusema: Anawatukusa watu akifundisha katika Yudea yote; naye ameanza Galilea, akafika mpaka hapa. 6Lakini Pilato alipoyasikia haya akauliza, kama ni mtu wa Galilea. 7Naye alipotambua, ya kuwa alitoka katika ufalme wa Herode, akamtuma kwa Herode, kwani naye alikuwako Yerusalemu siku zile.#Luk. 3:1.
Herode.
8Herode alipomwona Yesu akafurahi sana; kwani tangu siku nyingi alikuwa akitaka kumwona, kwa sababu aliyasikia mambo yake, akangojea kuona kielekezo kinachofanyizwa naye.#Luk. 9:9. 9Akamwuliza mengi, lakini yeye hakumjibu neno.#Luk. 13:31-32. 10Lakini watambikaji wakuu na waandishi waliosimama hapo wakajihimiza kumsuta. 11Herode pamoja na askari wake walipokwisha kumbeza na kumfyoza, akamvika nguo nyeupe imetukayo, akamrudisha kwa Pilato! 12Siku ile Herode na Pilato walianza kuwa rafiki, maana siku zilizopita walikuwa wanachukiana.
Kuhukumiwa.
13Pilato akawaita watambikaji wakuu na wakubwa na watu wa kwao, wakutane, 14akawaambia: Mmemleta kwangu mtu huyu, kwamba anawapindua watu; tazameni, mimi nimemwulizauliza mbele yenu, nisione kwake mtu huyu, ya kuwa ameyakosa, mnayomsuta. 15Hata Herode vile vile hakuona, kwani amemrudisha kwetu. Tazameni, hakukosa neno limpasalo kuuawa. 16Basi, nitampiga, kisha nitamfungua. 17Maana ilikuwa imempasa kuwafungulia mmoja kwa desturi ya sikukuu. 18Watu wote pia wakapiga kelele wakisema: Umwondoe huyu, afe, utufungulie Baraba! 19Naye Baraba alikuwa ametiwa kifungoni kwa ajili ya kondo iliyokuwamo mjini na kwa ajili ya kuua watu. 20Pilato akasema nao tena, kwani alitaka kumfungua Yesu. 21Lakini wakabisha wakisema: Mwambe msalabani! Mwambe msalabani! 22Ndipo, alipowauliza mara ya tatu: Ni kiovu gani, alichokifanya huyu? Sikuona neno kwake la kumhukumu, auawe; basi, nitampiga, kisha nitamfungua. 23Lakini wale wakamchokesha kwa kupiga makelele sana wakitaka, awambwe msalabani; ndivyo, makelele yao nayo ya watambikaji wakuu yalivyoshinda. 24Pilato akakata shauri na kuyaitikia, waliyoyataka: 25akamfungua yule aliyetiwa kifungoni kwa ajili ya kondo na ya kuua watu, ndiye waliyemtaka; lakini Yesu akamtoa, wamfanyizie watakavyo.
Wanawake wa Yerusalemu.
(26: Mat. 27:32; Mar. 15:21.)
26Walipompeleka wakamshika Simoni wa Kirene aliyepita akitoka shambani, wakamtwika msalaba, amchukulie Yesu na kumfuata.
27*Wakamfuata watu wengi mno, hata wanawake waliojipigapiga vifua na kumlilia. 28Yesu akawageukia, akasema: Enyi wanawake wa Yerusalemu, msinililie mimi, ila mjililie wenyewe na watoto wenu! 29Kwani tazameni, siku zitakuja, watakaposema: Wenye shangwe ndio wagumba na matumbo yasiyozaa na maziwa yasiyonyonyesha!#Luk. 21:23. 30Ndipo, watakapoanza kuiambia milima: Tuangukieni! na kuyaambia machuguu: Tufunikeni!#Hos. 10:8; Ufu. 6:16; 9:6. 31Kwani mti mbichi wakiufanyizia hivyo huo mkavu utakuwaje?#1 Petr. 4:17.
Kumwamba Yesu msalabani.
32Wakapelekwa nao wengine wawili waliofanya maovu, wauawe pamoja naye.
(33-49: Mat. 27:33-56; Mar. 15:22-41; Yoh. 19:17-30.)
33Walipofika mahali panapoitwa Fuvu la Kichwa, wakamwamba msalabani pale yeye na wale wafanya maovu, mmoja kuumeni, mmoja kushotoni. 34Kisha Yesu akasema: Baba, waondolee! Kwani hawajui wafanyayo.* Hata nguo zake wakazipigia kura, wazigawanyiane.#Sh. 22:19; Yes. 53:12; Mat. 5:44; Tume. 3:17; 7:60.
35Nao watu walikuwa wamesimama wakitazama; lakini wakuu wakamfyoza wakisema: Wengine aliwaokoa, na ajiokoe mwenyewe, kama ndiye Kristo aliyechaguliwa na Mungu! 36Nao askari wakamfyoza wakimkaribia na kumpelekea siki 37wakisema: Kama ndiwe mfalme wa Wayuda, jiokoe! 38Tena juu yake palikuwa pameandikwa Kigriki na Kiroma na Kiebureo: HUYU NDIYE MFALME WA WAYUDA.
Wafanya maovu wawili.
39*Mwenzao mmoja wale wafanya maovu waliotundikwa akambeza: Wewe siwe Kristo? Jiokoe mwenyewe na sisi! 40Lakini mwenzake akajibu akimkaripia na kusema: Humwogopi Mungu wewe nawe, uliomo katika mapatilizo yaya haya? 41Na sisi tumehukumiwa kweli, kwani tunalipizwa yaliyoyapasa matendo yetu; lakini huyu hakuna kipotovu, alichokifanya. 42Kisha akasema: Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako!#Mat. 16:28. 43Yesu akamwambia: Kweli nakuambia: Leo utakuwa pamoja nami katika Paradiso.
Kufa kwa Yesu.
44Ikawa, ilipofika kama saa sita, pakawa na giza katika nchi yote nzima mpaka saa tisa, 45kwa kuwa jua liliacha kuwaka; ndipo, pazia la Jumbani mwa Mungu lilipopasuka katikati.#2 Mose 36:35. 46Yesu akapaza sauti kuu akisema: Baba, roho yangu naiweka mikononi mwako. Alipokwisha kuyasema haya, pumzi ikamtoka.*#Sh. 31:6; Tume. 7:59.
47Lakini bwana askari alipoliona lililokuwapo akamtukuza Mungu akisema: Kweli mtu huyu alikuwa mwongofu. 48Nayo makundi yote ya watu waliokuwako kuyatazama hayo, walipoyaona yaliyokuwapo wakarudi kwao na kujipiga vifua. 49Nao wote waliojuana naye walikuwa wamesimama mbali, hata wanawake waliofuatana naye toka Galilea walikuwako wakiyatazama hayo.#Luk. 8:2-3.
Kumzika Yesu.
(50-56: Mat. 27:57-61; Mar. 15:42-47; Yoh. 19:38-42.)
50Ndipo, palipotokea mtu aliyekuwa mkuu, jina lake Yosefu wa Arimatia, ndio mji wa Wayuda. Huyo alikuwa mtu mwema na mwongofu; 51kwa hiyo hakujitia katika mashauri na matendo yao; naye alikuwa akiungoja ufalme wa Mungu.#Luk. 2:25,38. 52Huyo akaenda kwa Pilato, akataka kupewa mwili wa Yesu. 53Akaushusha msalabani, akaufunga kwa sanda, akauweka katika kaburi lililochongwa mwambani, ambalo hajazikwa mtu bado ndani yake. 54Nayo siku ile ilikuwa ya andalio; ndipo, sikukuu ilipoanzia. 55Lakini wanawake waliokuja pamoja naye toka Galilea wakafuata, wakalitazama kaburi, tena jinsi mwili wake ulivyowekwa.#Luk. 23:49. 56Kisha wakarudi, wakatengeneza viungo na manukato; lakini siku ya mapumziko wakakaa kimya, kama walivyoagizwa.#2 Mose 20:10.
Trenutno izabrano:
Luka 23: SRB37
Istaknuto
Podijeli
Kopiraj
Želiš li da tvoje istaknuto bude sačuvano na svim tvojim uređajima? Kreiraj nalog ili se prijavi
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.