Hivyo Eli akamwambia Samweli, “Nenda ukalale, na kama akikuita, sema, ‘Nena BWANA, kwa kuwa mtumishi wako anasikiliza.’ ” Hivyo Samweli akaenda na kulala mahali pake.
BWANA akaja akasimama hapo, akiita kama mara zile nyingine, “Samweli! Samweli!”
Kisha Samweli akasema, “Nena BWANA, kwa kuwa mtumishi wako anasikiliza.”