Haya yote yanatokana na Mungu, ambaye ametupatanisha sisi na nafsi yake kupitia kwa Isa Al-Masihi, na kutupatia sisi huduma ya upatanisho: kwamba Mungu alikuwa ndani ya Al-Masihi akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake mwenyewe, akiwa hawahesabii watu dhambi zao. Naye ametukabidhi sisi ujumbe huu wa upatanisho.