1
2 Wakorintho 4:18
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Kwa hivyo hatuangalii yale yanayoonekana, bali yale yasiyoonekana. Kwa maana yale yanayoonekana ni ya kitambo tu, bali yale yasiyoonekana ni ya milele.
Linganisha
Chunguza 2 Wakorintho 4:18
2
2 Wakorintho 4:16-17
Kwa hiyo, hatukati tamaa. Ingawa utu wetu wa nje unachakaa, utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Kwa maana dhiki yetu nyepesi iliyo ya kitambo inatutayarisha kwa ajili ya utukufu wa milele unaozidi kuwa mwingi kupita kiasi.
Chunguza 2 Wakorintho 4:16-17
3
2 Wakorintho 4:8-9
Twataabika kila upande lakini hatuangamizwi; twaona wasiwasi lakini hatukati tamaa; twateswa lakini hatuachwi; twatupwa chini lakini hatupondwi.
Chunguza 2 Wakorintho 4:8-9
4
2 Wakorintho 4:7
Lakini tunayo hazina hii katika vyombo vya udongo, ili ijulikane wazi kwamba uwezo huu wa ajabu unatoka kwa Mungu, wala si kwetu.
Chunguza 2 Wakorintho 4:7
5
2 Wakorintho 4:4
Kwa habari yao, mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Al-Masihi, aliye sura ya Mungu.
Chunguza 2 Wakorintho 4:4
6
2 Wakorintho 4:6
Kwa kuwa Mungu, yeye aliyesema, “Nuru na ing’ae gizani,” ameifanya nuru yake ing’ae mioyoni mwetu ili kutupatia nuru ya maarifa ya utukufu wa Mungu katika uso wa Al-Masihi.
Chunguza 2 Wakorintho 4:6
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video