Yeye aendaye kwa uadilifu
na kusema lililo haki,
yeye anayekataa faida ipatikanayo kwa dhuluma
na kuizuia mikono yake isipokee rushwa,
yeye azuiaye masikio yake dhidi ya mashauri ya mauaji,
na yeye afumbaye macho yake yasitazame sana uovu:
huyu ndiye mtu atakayeishi mahali pa juu,
ambaye kimbilio lake litakuwa ngome ya mlimani.
Atapewa mkate wake,
na maji yake hayatakoma.