1
Isaya 45:3
Neno: Bibilia Takatifu
Nitakupa hazina za gizani, mali zilizofichwa mahali pa siri, ili upate kujua ya kwamba Mimi ndimi BWANA, Mungu wa Israeli, akuitaye kwa jina lako.
Linganisha
Chunguza Isaya 45:3
2
Isaya 45:2
Nitakwenda mbele yako na kusawazisha milima; nitavunjavunja malango ya shaba na kukatakata mapingo ya chuma.
Chunguza Isaya 45:2
3
Isaya 45:5-6
Mimi ndimi BWANA, wala hakuna mwingine, zaidi yangu hakuna Mungu. Nitakutia nguvu, ingawa wewe hujanitambua, ili kutoka mawio ya jua mpaka machweo yake, watu wapate kujua kwamba hakuna Mungu mwingine ila Mimi. Mimi ndimi BWANA wala hakuna mwingine.
Chunguza Isaya 45:5-6
4
Isaya 45:7
Mimi ninaumba nuru na kuhuluku giza, ninaleta mafanikio na kusababisha maafa. Mimi, BWANA, huyatenda haya yote.
Chunguza Isaya 45:7
5
Isaya 45:22
“Nigeukieni mimi, nanyi mkaokolewe, enyi miisho yote ya dunia; kwa maana mimi ndimi Mungu, wala hapana mwingine.
Chunguza Isaya 45:22
6
Isaya 45:1
“Hili ndilo asemalo BWANA kwa mpakwa mafuta wake, Koreshi, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume kutiisha mataifa mbele yake na kuwavua wafalme silaha zao, kufungua milango mbele yake ili malango yasije yakafungwa
Chunguza Isaya 45:1
7
Isaya 45:23
Nimeapa kwa nafsi yangu, kinywa changu kimenena katika uadilifu wote neno ambalo halitatanguka: Kila goti litapigwa mbele zangu, kwangu mimi kila ulimi utaapa.
Chunguza Isaya 45:23
8
Isaya 45:4
Kwa ajili ya Yakobo mtumishi wangu, Israeli niliyemchagua, nimekuita wewe kwa jina lako, na kukupa jina la heshima, ingawa wewe hunitambui.
Chunguza Isaya 45:4
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video