1
Isaya 6:8
Neno
NEN
Kisha nikasikia sauti ya Bwana ikisema, “Nimtume nani? Ni nani atakayeenda kwa ajili yetu?” Nami nikasema, “Mimi hapa. Nitume mimi!”
Linganisha
Chunguza Isaya 6:8
2
Isaya 6:3
Nao walikuwa wakiitana kila mmoja na mwenzake: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni BWANA wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.”
Chunguza Isaya 6:3
3
Isaya 6:5
Ndipo nikalia, “Ole wangu! Nimeangamia! Kwa kuwa mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninaishi kati ya watu wenye midomo michafu, nayo macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi.”
Chunguza Isaya 6:5
4
Isaya 6:1
Katika mwaka ule Mfalme Uzia alikufa, nilimwona Bwana ameketi kwenye kiti cha enzi, kilicho juu na kilichotukuzwa sana, nalo pindo la joho lake likajaza Hekalu.
Chunguza Isaya 6:1
5
Isaya 6:7
Akanigusa nalo kinywa changu na kusema, “Tazama, hili limegusa midomo yako, uovu wako umeondolewa, nayo dhambi yako imesamehewa.”
Chunguza Isaya 6:7
6
Isaya 6:2
Juu yake walikuwa maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita: Kwa mabawa mawili walifunika nyuso zao, kwa mengine mawili walifunika miguu yao, na kwa mawili walikuwa wakiruka.
Chunguza Isaya 6:2
7
Isaya 6:6
Ndipo mmoja wa wale maserafi akaruka kunijia akiwa na kaa la moto linalowaka mkononi mwake, ambalo alikuwa amelichukua kwa koleo kutoka madhabahuni.
Chunguza Isaya 6:6
8
Isaya 6:9
Akasema, “Nenda ukawaambie watu hawa: “ ‘Mtaendelea daima kusikiliza, lakini kamwe hamtaelewa; mtaendelea daima kutazama, lakini kamwe hamtatambua.’
Chunguza Isaya 6:9
9
Isaya 6:10
Fanya mioyo ya watu hawa kuwa migumu, fanya masikio yao yasisikie, na upofushe macho yao. Wasije wakaona kwa macho yao, na wakasikiliza kwa masikio yao, wakaelewa kwa mioyo yao, nao wakageuka, wakaponywa.”
Chunguza Isaya 6:10