1
Mithali 16:3
Neno: Bibilia Takatifu
Mkabidhi BWANA lolote ufanyalo, nayo mipango yako itafanikiwa.
Linganisha
Chunguza Mithali 16:3
2
Mithali 16:9
Moyo wa mtu huifikiri njia yake, bali BWANA huelekeza hatua zake.
Chunguza Mithali 16:9
3
Mithali 16:24
Maneno ya kupendeza ni kama sega la asali, ni matamu kwa nafsi na uponyaji kwenye mifupa.
Chunguza Mithali 16:24
4
Mithali 16:1
Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu, bali jibu la ulimi hutoka kwa BWANA.
Chunguza Mithali 16:1
5
Mithali 16:32
Ni afadhali mtu mstahimilivu kuliko shujaa, mtu anayeitawala hasira yake kuliko yule autekaye mji.
Chunguza Mithali 16:32
6
Mithali 16:18
Kiburi hutangulia maangamizi, roho ya majivuno hutangulia maanguko.
Chunguza Mithali 16:18
7
Mithali 16:2
Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe, bali makusudi hupimwa na BWANA.
Chunguza Mithali 16:2
8
Mithali 16:20
Yeyote anayekubali mafundisho hustawi, tena amebarikiwa yeye anayemtumaini BWANA.
Chunguza Mithali 16:20
9
Mithali 16:8
Afadhali kitu kidogo pamoja na haki kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu.
Chunguza Mithali 16:8
10
Mithali 16:25
Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu, bali mwisho wake huelekeza mautini.
Chunguza Mithali 16:25
11
Mithali 16:28
Mtu mpotovu huchochea ugomvi, nayo maongezi ya upuzi hutenganisha marafiki wa karibu.
Chunguza Mithali 16:28
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video