1
Ufunuo 5:9
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Nao wakaimba wimbo mpya, wakisema: “Wewe unastahili kukitwaa kitabu na kuivunja mihuri yake, kwa sababu ulichinjwa, na kwa damu yako ukamnunulia Mungu watu kutoka kila kabila, kila lugha, kila jamaa na kila taifa.
Linganisha
Chunguza Ufunuo 5:9
2
Ufunuo 5:12
Nao waliimba kwa sauti kuu, wakisema: “Anastahili Mwana-Kondoo, yeye aliyechinjwa, kupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na sifa!”
Chunguza Ufunuo 5:12
3
Ufunuo 5:10
Wewe umewafanya hawa wawe ufalme na makuhani wa kumtumikia Mungu wetu, nao watatawala duniani.”
Chunguza Ufunuo 5:10
4
Ufunuo 5:13
Kisha nikasikia kila kiumbe mbinguni na duniani, chini ya nchi, na baharini, na vyote vilivyomo, vikiimba: “Sifa na heshima na utukufu na uweza ni vyake yeye aliyeketi juu ya hicho kiti cha enzi, na kwa Mwana-Kondoo, milele na milele!”
Chunguza Ufunuo 5:13
5
Ufunuo 5:5
Kisha, mmoja wa wale wazee akaniambia, “Usilie! Tazama, Simba wa kabila la Yuda, wa Uzao wa Daudi, ameshinda. Yeye ndiye anayeweza kukifungua hicho kitabu na kuvunja mihuri yake saba.”
Chunguza Ufunuo 5:5
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video