1
Ufunuo 8:1
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Mwana-Kondoo alipouvunja ule muhuri wa saba, pakawa kimya mbinguni kwa muda wa nusu saa.
Linganisha
Chunguza Ufunuo 8:1
2
Ufunuo 8:7
Malaika wa kwanza akaipiga tarumbeta yake, pakatokea mvua ya mawe na moto uliochanganyika na damu, navyo vikatupwa kwa nguvu juu ya nchi. Na theluthi ya dunia ikateketea, theluthi ya miti ikateketea, na nyasi yote mbichi ikateketea.
Chunguza Ufunuo 8:7
3
Ufunuo 8:13
Nilipokuwa tena nikitazama, nikamsikia tai mmoja akipaza sauti kwa nguvu, huku akiruka katikati ya anga, akasema, “Ole! Ole! Ole wa watu wanaoishi duniani, kwa sababu ya tarumbeta ambazo malaika hao wengine watatu wanakaribia kuzipiga!”
Chunguza Ufunuo 8:13
4
Ufunuo 8:8
Malaika wa pili akaipiga tarumbeta yake na kitu kama mlima mkubwa unaowaka moto kikatupwa baharini. Theluthi ya bahari ikawa damu
Chunguza Ufunuo 8:8
5
Ufunuo 8:10-11
Malaika wa tatu akaipiga tarumbeta yake, na nyota kubwa iliyokuwa ikiwaka kama taa ikaanguka toka angani, ikaangukia theluthi ya mito na chemchemi za maji. Nyota hiyo inaitwa Pakanga. Theluthi ya maji yakawa machungu na watu wengi wakafa kutokana na maji hayo kwa maana yalikuwa machungu.
Chunguza Ufunuo 8:10-11
6
Ufunuo 8:12
Kisha malaika wa nne akaipiga tarumbeta yake, na theluthi ya jua, theluthi ya mwezi na theluthi ya nyota zikapigwa. Kwa hiyo theluthi moja ya mwanga ikawa giza. Theluthi ya mchana ikawa haina mwanga na pia theluthi ya usiku.
Chunguza Ufunuo 8:12
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video