1
Warumi 7:25
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Namshukuru Mungu anayeniokoa kupitia kwa Isa Al-Masihi Bwana wetu! Hivyo basi, mimi mwenyewe kwa akili zangu ni mtumwa wa Torati ya Mungu, lakini katika asili ya dhambi ni mtumwa wa sheria ya dhambi.
Linganisha
Chunguza Warumi 7:25
2
Warumi 7:18
Kwa maana ninafahamu kwamba hakuna jema lolote linalokaa ndani yangu, yaani katika asili yangu ya dhambi. Kwa kuwa nina shauku ya kutenda lililo jema, lakini siwezi kulitenda.
Chunguza Warumi 7:18
3
Warumi 7:19
Sitendi lile jema nitakalo kutenda, bali lile baya nisilolitaka, ndilo nitendalo.
Chunguza Warumi 7:19
4
Warumi 7:20
Basi kama ninatenda lile nisilotaka kutenda, si mimi tena nifanyaye hivyo, bali ni ile dhambi inayokaa ndani yangu.
Chunguza Warumi 7:20
5
Warumi 7:21-22
Hivyo naiona Torati ikitenda kazi. Ninapotaka kutenda jema, jambo baya liko papo hapo. Kwa maana katika utu wangu wa ndani naifurahia Torati ya Mungu.
Chunguza Warumi 7:21-22
6
Warumi 7:16
Basi kama ninatenda lile nisilotaka kutenda, ni kwamba ninakubali kuwa Torati ni njema.
Chunguza Warumi 7:16
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video