Katika ndoto, katika maono ya usiku,
Usingizi mzito uwajiapo watu,
Katika usingizi kitandani;
Ndipo huyafunua masikio ya watu,
Na kuyatia mhuri mafundisho yao,
Ili amwondoe mtu katika makusudio yake,
Na kumfichia mtu kiburi;
Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni,
Na uhai wake usiangamie kwa upanga.