Yobu 33:15-18
Yobu 33:15-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu huongea na watu katika ndoto na maono, wakati usingizi mzito unapowavamia, wanaposinzia vitandani mwao. Hapo huwafungulia watu masikio yao; huwatia hofu kwa maonyo yake, wapate kuachana na matendo yao mabaya, na kuvunjilia mbali kiburi chao. Hivyo humkinga mtu asiangamie shimoni, maisha yake yasiangamie kwa upanga.
Yobu 33:15-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiapo watu, Katika usingizi kitandani; Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia mhuri mafundisho yao, Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga.
Yobu 33:15-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao, Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga.
Yobu 33:15-18 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mungu husema na mwanadamu katika ndoto, katika maono ya usiku, wakati usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu wasinziapo vitandani mwao, anaweza akasemea masikioni mwao, na kuwatia hofu kwa maonyo, ili kumgeuza mtu kutoka kwenye kutenda mabaya na kumwepusha na kiburi, kuiokoa nafsi yake na shimo, uhai wake usiangamizwe kwa upanga.