1
Warumi 7:25
Swahili Revised Union Version
Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.
Linganisha
Chunguza Warumi 7:25
2
Warumi 7:18
Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema siwezi.
Chunguza Warumi 7:18
3
Warumi 7:19
Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.
Chunguza Warumi 7:19
4
Warumi 7:20
Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
Chunguza Warumi 7:20
5
Warumi 7:21-22
Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya. Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani
Chunguza Warumi 7:21-22
6
Warumi 7:16
Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema.
Chunguza Warumi 7:16
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video