1
Yohana 3:16
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Kweli, hivi ndivyo Mungu alivyouonyesha upendo wake mkuu kwa ulimwengu: akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu anayemwamini asiharibiwe na mauti bali aupate uzima wa milele.
Linganisha
Chunguza Yohana 3:16
2
Yohana 3:17
Mungu alimtuma Mwanawe ili kuuokoa ulimwengu. Hakumtuma kuja kuuhukumu na kuuweka hatiani, bali kuuokoa kwa njia ya mwanawe.
Chunguza Yohana 3:17
3
Yohana 3:3
Yesu akajibu, “Hakika nakuambia, ni lazima kila mtu azaliwe upya. Yeyote ambaye hajazaliwa mara ya pili hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu.”
Chunguza Yohana 3:3
4
Yohana 3:18
Wote wanaomwamini Mwana wa Mungu hawahukumiwi hatia yoyote. Lakini wale wasiomwamini wamekwisha kuhukumiwa tayari, kwa sababu hawakumwamini Mwana pekee wa Mungu.
Chunguza Yohana 3:18
5
Yohana 3:19
Wamehukumiwa kutokana na ukweli huu: Kwamba nuru imekuja ulimwenguni, lakini watu hawakuitaka nuru. Bali walilitaka giza, kwa sababu walikuwa wanatenda mambo maovu.
Chunguza Yohana 3:19
6
Yohana 3:30
Yeye anapaswa kuwa juu zaidi yangu mimi, na mimi napaswa kuwa chini yake kabisa.”
Chunguza Yohana 3:30
7
Yohana 3:20
Kila anayetenda maovu huichukia nuru. Hawezi kuja kwenye nuru, kwa sababu nuru itayaweka wazi matendo maovu yote aliyotenda.
Chunguza Yohana 3:20
8
Yohana 3:36
Yeyote anayemwamini Mwana anao uzima wa milele. Lakini wale wasiomtii Mwana hawataupata huo uzima. Na hawataweza kuiepuka hasira ya Mungu.”
Chunguza Yohana 3:36
9
Yohana 3:14
Unakumbuka yule nyoka wa shaba ambaye Musa alimwinua kule jangwani? Vivyo hivyo Mwana wa Adamu anapaswa kuinuliwa juu.
Chunguza Yohana 3:14
10
Yohana 3:35
Baba anampenda Mwana na amempa uwezo juu ya kila kitu.
Chunguza Yohana 3:35
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video