Alipokwisha kukawia kwao siku kumi na zaidi, akatelemkia Kaisaria: hatta siku ya pili akaketi katika kiti cha hukumu akaamuru Paolo aletwe. Walipokuja Wayahudi walioshuka kutoka Yerusalemi wakasimama karibu yake wakaleta mashitaka mengi na mazito juu yake, wasiyoweza kuyathuhutisha.