wakawaambia: Afadhali tungalikufa katika nchi ya Misri kwa kupigwa na mkono wa Bwana. Huko tulikaa na masufuria yenye nyama, tukapata vyakula vya kushiba, kwani mmetutoa huko na kutuleta huku nyikani, mwaue kwa njaa wao wote walio wa mkutano huu.
Ndipo, Bwana alipomwambia Mose: Mtaniona, nikiwanyeshea ninyi mvua ya mikate toka mbinguni, watu watoke tu kuiokota kila siku iipasayo hiyo siku, nipate kuwajaribu, kama wataendelea kuyashika maonyo yangu, au kama sivyo.