Ikawa, Mose alipouinua mkono wake, Waisiraeli wakashinda; lakini alipoushusha mkono wake, upumzike, Waamaleki wakashinda. Mikono ya Mose ilipolegea kwa kuwa mizito, wakachukua jiwe, wakaliweka chini yake, apate kulikalia. Kisha Haroni na Huri wakaishikiza mikono yake, mmoja huku, mmoja huko; ndivyo, mikono yake ilivyopata nguvu, mpaka jua lilipokuchwa