2 Mose 17
17
Mose anatoa maji mwambani.
1Wao wote wa mkutano wa wana wa Isiraeli wakaondoka katika nyika ya sini kwenda safari zao kwa kuagizwa na Bwana, wakapiga makambi Refidimu, lakini maji ya kunywa watu hayakuwako. 2Ndipo, watu walipomgombeza Mose na kusema: Tupeni maji, tunywe! Mose akawaambia: Mbona mnanigombeza? Mbona mnamjaribu Bwana?#5 Mose 6:16; 1 Kor. 10:9. 3Lakini hawa watu kwa kuwa waliona huko kiu ya maji, wakamnung'unikia Mose kwamba: Kwa nini umetutoa kule Misri, utuue kwa kiu sisi na wana wetu na makundi yetu?#4 Mose 14:10. 4Naye Mose akamlilia Bwana kwamba: Watu hawa niwafanyie nini? Kidogo tena, wangenipiga mawe. 5Bwana akamwambia Mose: Pita mbele ya hawa watu, uchukue wazee wengine wa Waisiraeli kwenda pamoja na wewe, nayo ile fimbo yako iliyoupiga ule mto ishike mkononi mwako, kisha nenda!#2 Mose 7:20. 6Utakaponiona, nikisimama mbele yako mwambani juu huko Horebu, uupige huo mwamba; ndipo, utakapotoka maji, watu wanywe. Mose akayafanya vivyo hivyo machoni pa wazee wa Kiisiraeli,#4 Mose 20:11; 1 Kor. 10:4. 7akapaita Masa na Meriba (Majaribu na Magomvi), kwa kuwa wana wa isiraeli walimgombeza hapo, wakamjaribu naye Bwana wakisema: Je? Bwana yumo katikati yetu au hayumo?#Sh. 95:8-9.
Waamaleki wanashindwa.
8Waamaleki wakaja kupigana nao Waisiraeli huko Refidimu.#4 Mose 13:8,16. 9Ndipo, Mose alipomwambia Yosua: Utuchagulie waume, utoke nao kupigana na Waamaleki! Mimi nami nitasimama kesho juu ya hiki kilima, nayo fimbo ya Mungu itakuwa mkononi mwangu. 10Yosua akafanya, kama Mose alivyomwagiza kwenda kupigana na Waamaleki, lakini Mose na Haroni na Huri wakakipanda hicho kilima, mpaka wafike juu. 11Ikawa, Mose alipouinua mkono wake, Waisiraeli wakashinda; lakini alipoushusha mkono wake, upumzike, Waamaleki wakashinda. 12Mikono ya Mose ilipolegea kwa kuwa mizito, wakachukua jiwe, wakaliweka chini yake, apate kulikalia. Kisha Haroni na Huri wakaishikiza mikono yake, mmoja huku, mmoja huko; ndivyo, mikono yake ilivyopata nguvu, mpaka jua lilipokuchwa, 13tena ndivyo, Yosua alivyowashinda Waamaleki na watu wao kwa ukali wa panga.
14Bwana akamwambia Mose: Yaandike haya katika kitabu, yakumbukwe siku zote! Tena mwelezee Yosua, ya kama nitafuta kabisa ukumbusho wote wa Waamaleki, watoweke chini ya mbingu.#5 Mose 25:17-19; 1 Sam. 15:2-3. 15Kisha Mose akajenga pa kumtambikia Bwana, akapaita jina lake: Bwana ni Bendera yangu, 16kwani alisema: Bwana ameuweka mkono penye bendera kwamba: Bwana atapiga vita na Waamaleki kwa vizazi na vizazi.
Iliyochaguliwa sasa
2 Mose 17: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.