Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Mose 18

18
Yetoro, mkwewe Mose, anaamkiana naye.
1Yetoro, mtambikaji wa Midiani, aliyekuwa mkwewe Mose, alipoyasikia yote, Mungu aliyomfanyizia Mose nao ukoo wake wa Waisiraeli, ya kuwa Bwana aliwatoa Waisiraeli huko Misri,#2 Mose 3:1. 2ndipo, Yetoro, mkwewe Mose, alipomchukua Sipora, mkewe Mose, aliyemrudisha,#2 Mose 4:20. 3na wanawe wawili, mmoja jina lake Gersomu (Mgeni wa Huku), kwani alisema: Mimi nimekuwa mgeni katika nchi isiyo ya kwetu;#2 Mose 2:22. 4naye wa pili jina lake Eliezeri (Mungu Msaada wangu), kwani alisema: Mungu wa baba yangu amenisaidia, ameniponya upanga wa Farao. 5Yetoro, mkwewe Mose, alipofika pamoja na wanawe na mkewe kwake Mose huko nyikani, alikokuwa amepanga kwenye mlima wa Mungu, 6akatuma kumwambia Mose: Mimi mkweo Yetoro nimekuja kwako pamoja na mkeo na wanawe wawili. 7Ndipo, Mose alipotoka kumwendea njiani, akamwinamia, akanoneana naye, nao wakatakiana kuwa hawajambo, kisha wakaingia hemani. 8Mose akamsimulia mkwewe yote, Bwana aliyomfanyizia Farao nao Wamisri kwa ajili ya Waisiraeli, nayo masumbuko yote yaliyowapata njiani, tena jinsi Bwana alivyowaponya. 9Yetoro akayafurahia hayo mema yote, Bwana aliyowafanyizia Waisiraeli na kuwaponya mikononi mwa Wamisri. 10Kisha Yetoro akasema: Bwana na atukuzwe aliyewaponya mikononi mwa Wamisri namo mkononi mwa Farao, kwa kuwa amewaponya watu hawa na kuwatoa mikononi mwa Wamisri! 11Sasa ninatambua, ya kuwa Bwana ni mkuu kuliko miungu yote, nao wale walikuwa wamejivunia ukuu wao kwao hawa.#Neh. 9:10. 12Naye Yetoro, mkwewe Mose, akamtolea Mungu ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na za kuchinjwa, naye Haroni nao wazee wote wa Waisiraeli wakaja kula chakula pamoja na mkwewe Mose mbele ya Mungu.
Kuweka wenye kukata mashauri ya watu.
13Kesho yake asubuhi Mose akakaa kuwaamua watu, nao watu wakasimama kwake Mose toka asubuhi hata jioni. 14Mkwewe Mose alipoyaona yote, aliyowafanyia watu, akasema: Hili jambo linakuwaje, ukijisumbua hivyo na hawa watu? Mbona wewe unakaa peke yako, nao hawa watu wanasimama kwako toka asubuhi hata jioni? 15Naye Mose akamwambia mkwewe: Hawa watu wakija kwangu, ni kwa kuwa wanataka kumwuliza Mungu. 16Wakipatwa na shauri huja kwangu, niwaamue wao kwa wao na kuwajulisha maongozi ya Mungu na maonyo yake. 17Naye mkwewe Mose akamwambia: Hivyo, unavyolifanya jambo hili, havifai. 18Hivyo wewe mwenyewe utalegea kwa uchovu nao watu hao, ulio nao, kwani kazi hii ni ngumu zaidi ya kukushinda, huwezi kuifanya peke yako.#4 Mose 11:14; 5 Mose 1:9. 19Sasa isikie sauti yangu, nikupe shauri, naye Mungu na awe pamoja na wewe! Wewe wasemee watu mbele ya Mungu na kuyapeleka mashauri yao kwake Mungu! 20Tena uwafundishe maongozi na kuwajulisha njia, watakayoishika, nayo matendo, watakayoyafanya. 21Lakini tena ujitazamie kwa watu wote wana waume wenye nguvu wamchao Mungu kwa kweli, wachukiao kupenyezewa, wao uwaweke kuwa wakuu wa maelfu na wakuu wa mamia na wakuu wa hamsini na wakuu wa makumi, 22wawaamue watu siku zote, kwako walete mashauri makubwa tu, lakini mashauri madogo yote wayakate wao! Hivi mzigo wako utapunguka, wao wakikusaidia kuuchukua. 23Ukivifanya hivyo, naye Mungu akikuagiza hivyo, wewe utaweza kujitunza, nao watu hawa wote wataweza kwenda zao na kutengemana. 24Mose akaisikia sauti ya mkwewe, akayafanya yote, aliyoyasema. 25Kwa hiyo Mose akachagua kwa Waisiraeli wote watu wenye nguvu, akawaweka kuwa vichwa vya watu hawa, maana wakuu wa maelfu na wakuu wa mamia na wakuu wa hamsini na wakuu wa makumi, 26wawaamue watu siku zote, lakini mashauri magumu wayalete kwake yeye Mose, lakini mashauri madogo wayakate wao. 27Kisha Mose akamsindikiza mkwewe, akaenda zake katika nchi yake.

Iliyochaguliwa sasa

2 Mose 18: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia