Siku sita sharti ufanye kazi, uyamalize mambo yako yote! Lakini siku ya saba ndiyo ya kumpumzikia Bwana Mungu wako. Hapo usifanye kazi yo yote, wala wewe, wala mwanao wa kiume, wala wa kike, wala mtumishi wako wa kiume, wala wa kike, wala nyama wako wa kufuga, wala mgeni wako aliomo malangoni mwako.