Ndipo, Mungu alipomwambia katika ndoto: Mimi nami nimejua, ya kama umevifanya hivyo kwa moyo usiovijua kuwa vibaya. Kwa sababu hii mimi nami nimekuzuia, usinikosee, nikakukataza kumgusa. Sasa mrudishie yule mtu mkewe! Kwani ni mfumbuaji, akuombee, upate kupona; lakini usipomrudisha, ujue, ya kuwa utakufa kweli, wewe pamoja nao wote walio wako.