Mungu alipokisikia kilio cha mtoto, malaika wa Mungu akamwita Hagari toka mbinguni, akamwambia: Una nini, Hagari? Usiogope! Kwani Mungu amekisikia kilio cha mtoto hapo, anapolala. Inuka, umwinue mtoto na kumshika kwa mkono wako! Kwani nitamfanya kuwa taifa kubwa.