1 Mose 20
20
Aburahamu na Sara na Abimeleki.
1Kisha aburahamu akaondoka huko kwenda katika nchi ya upande wa kusini, akakaa ugenini katikati ya Kadesi na Suri huko Gerari.#1 Mose 12:9-10; 26:1. 2Kwa ajili ya mkewe Sara Aburahamu akasema: Huyu ni dada yangu. Kwa hiyo Abimeleki, mfalme wa Gerari, akatuma watu kumchukua Sara. 3Ndipo, Mungu alipokuja kwa mfalme Abimeleki usiku katika ndoto, akamwambia: Tazama, utakufa kwa ajili ya huyu mwanamke, uliyemchukua, maana ni mke wa bwana mwingine. 4Naye Abimeleki alikuwa hajamkaribia bado, kwa hiyo akasema: Bwana, watu wasiokosa utawaua nao? 5Yule hakuniambia: Huyu ni dada yangu? Naye mwenyewe amesema: Yule ni kaka yangu. Hivyo nimevifanya kwa moyo usiojua kuwa vibaya na kwa mikono iliyotakata. 6Ndipo, Mungu alipomwambia katika ndoto: Mimi nami nimejua, ya kama umevifanya hivyo kwa moyo usiovijua kuwa vibaya. Kwa sababu hii mimi nami nimekuzuia, usinikosee, nikakukataza kumgusa. 7Sasa mrudishie yule mtu mkewe! Kwani ni mfumbuaji, akuombee, upate kupona; lakini usipomrudisha, ujue, ya kuwa utakufa kweli, wewe pamoja nao wote walio wako.#Sh. 105:15.
8Kesho yake abimeleki akaamka na mapema, akawaita watumishi wake wote, akayasema hayo maneno yote masikioni pao; ndipo, hao watu waliposhikwa na woga kabisa. 9Kisha Abimeleki akamwita Aburahamu, akamwambia: Kwa nini umetufanyia hivyo? Mimi nimekukosea nini, ukitaka kunikosesha sana mimi pamoja nao, ninaowatawala? Umenifanyizia mambo yasiyofanywa. 10Abimeleki akamwuliza Aburahamu: Umeona nini ukilifanya jambo hilo? 11Aburahamu akasema: Nimesema tu moyoni: Huku hakuna wenye kumwogopa Mungu, kwa hiyo wataniua kwa ajili ya mke wangu. 12Naye ni dada yangu kweli kwa kuwa mwana wa baba yangu, lakini si mwana wa mama yangu, kwa hiyo aliweza kuwa mke wangu. 13Ikawa hapo, Mungu aliponitoa nyumbani mwa baba yangu kusafiri huku na huko, nikamwambia: Unifanyie upendeleo huu, po pote tutakapofika, useme kwa ajili yangu: Huyu ni kaka yangu.
14Ndipo, Abimeleki alipochukua mbuzi na kondoo na ng'ombe na watumwa wa kiume na wa kike, akampa Aburahamu, akamrudishia mkewe Sara, 15akamwambia: Tazama, nchi yangu iko mbele yako, kaa palipo pema machoni pako! 16Naye Sara akamwambia: Tazama, kaka yako nimempa fedha elfu, upate kaya za kuwafunika ushungi wao wote, ulio nao; ndivyo, utakavyojulikana kwao wote kuwa mtu asiyekosa. 17Aburahamu alipomwomba Mungu, Mungu akamponya Abimeleki, naye mkewe, nao vijakazi wake, wakapata kuzaa tena. 18Kwani Bwana alikuwa ameyakomesha kuzaa matumbo yao wote wa mlango wa Abimeleki kwa ajili ya Sara, mkewe Aburahamu.
Iliyochaguliwa sasa
1 Mose 20: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.