1
Mwanzo 42:21
Neno: Maandiko Matakatifu
Wakaambiana wao kwa wao, “Hakika tunaadhibiwa kwa sababu ya ndugu yetu. Tuliona jinsi alivyohuzunika alipokuwa anatusihi kuponya maisha yake, lakini hatukumsikiliza, hiyo ndiyo sababu dhiki hii imetupata.”
Linganisha
Chunguza Mwanzo 42:21
2
Mwanzo 42:6
Wakati huo Yusufu alikuwa mtawala wa nchi ya Misri, naye alikuwa ndiye aliwauzia watu wote nafaka. Kwa hiyo wakati ndugu zake Yusufu walipofika, wakamsujudia hadi nyuso zao zikagusa ardhi.
Chunguza Mwanzo 42:6
3
Mwanzo 42:7
Mara Yusufu alipowaona ndugu zake, akawatambua, lakini akajifanya mgeni na kuzungumza nao kwa ukali, akiwauliza, “Ninyi mnatoka wapi?” Wakamjibu, “Tumetoka katika nchi ya Kanaani kuja kununua chakula.”
Chunguza Mwanzo 42:7
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video