1
Wakolosai 3:13
Biblia Habari Njema
Vumilianeni na kusameheana iwapo mmoja wenu analo jambo lolote dhidi ya mwenzake. Mnapaswa kusameheana kama Bwana alivyowasamehe nyinyi.
Linganisha
Chunguza Wakolosai 3:13
2
Wakolosai 3:2
Muwe na hamu ya mambo ya huko juu, na siyo mambo ya hapa duniani.
Chunguza Wakolosai 3:2
3
Wakolosai 3:23
Kila mfanyacho, fanyeni kwa moyo wote, kwa sababu ya Bwana na si kwa ajili ya mtu.
Chunguza Wakolosai 3:23
4
Wakolosai 3:12
Nyinyi ni watu wake Mungu; yeye aliwapenda na kuwateua. Kwa hiyo, basi, vaeni moyo wa huruma, wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.
Chunguza Wakolosai 3:12
5
Wakolosai 3:16-17
Ujumbe wa Kristo na ukae ndani yenu pamoja na utajiri wake wote. Fundishaneni na kushauriana kwa hekima yote. Imbeni Zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Mungu mioyoni mwenu kwa shukrani. Na, kila mfanyacho kwa neno au tendo, fanyeni vyote kwa jina la Bwana Yesu na kumshukuru Mungu Baba kwa njia yake.
Chunguza Wakolosai 3:16-17
6
Wakolosai 3:14
Zaidi ya hayo yote, zingatieni upendo, kwani upendo huunganisha kila kitu katika umoja ulio kamili.
Chunguza Wakolosai 3:14
7
Wakolosai 3:1
Basi, ikiwa mmefufuka pamoja na Kristo, panieni mambo ya juu, kule Kristo aliko, ameketi upande wa kulia wa Mungu.
Chunguza Wakolosai 3:1
8
Wakolosai 3:15
Nayo amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu; maana kwa ajili hiyo nyinyi mmeitwa katika mwili huo mmoja. Tena muwe na shukrani!
Chunguza Wakolosai 3:15
9
Wakolosai 3:5
Basi, ueni chochote kilicho ndani yenu ambacho ni cha kidunia: Uasherati, uchafu, shauku, tamaa mbaya na uchu (ambao ni sawa na kuabudu sanamu).
Chunguza Wakolosai 3:5
10
Wakolosai 3:3
Maana nyinyi mmekufa na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.
Chunguza Wakolosai 3:3
11
Wakolosai 3:8
Lakini sasa mnapaswa kuachana na mambo haya yote: Hasira, tamaa na uovu; kufuru au maneno yasiyofaa yasitoke kamwe vinywani mwenu.
Chunguza Wakolosai 3:8
12
Wakolosai 3:9-10
Msiambiane uongo, kwani nyinyi mmekwisha vua ule utu wa kale pamoja na matendo yake yote, mkavaa utu mpya. Huu unaendelea kurekebishwa na Mungu, Muumba wake, kadiri ya mfano wake, ili mpate kumjua Mungu kwa ukamilifu.
Chunguza Wakolosai 3:9-10
13
Wakolosai 3:19
Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali kwao.
Chunguza Wakolosai 3:19
14
Wakolosai 3:20
Enyi watoto, watiini wazazi wenu daima maana hiyo humpendeza Bwana.
Chunguza Wakolosai 3:20
15
Wakolosai 3:18
Enyi wake, watiini waume zenu, kwani ndivyo apendavyo Bwana.
Chunguza Wakolosai 3:18
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video