Ni mtu aishiye kwa uadilifu na asemaye ukweli;
mtu anayedharau kabisa utajiri wa dhuluma,
anayekataa hongo kata kata,
asiyekubali kamwe kusikia mipango ya mauaji,
wala hakubali macho yake yaone maovu.
Mtu wa namna hiyo anaishi juu,
mahali salama penye ngome na miamba;
chakula chake atapewa daima,
na maji yake ya kunywa hayatakosekana.