Lakini wao na babu zetu wakawa na kiburi
na wakawa na shingo ngumu
wakakataa kufuata maagizo yako.
Wakakataa kutii;
wasiyakumbuke maajabu uliyofanya miongoni mwao.
Wakawa na shingo zao ngumu,
wakajichagulia kiongozi wa kuwarudisha
utumwani nchini Misri.
Bali wewe Mungu u mwepesi kusamehe,
mwenye neema na huruma,
wewe hukasiriki upesi.
U mwenye fadhili nyingi, na hukuwatupa.