Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wakorintho 5

5
Mwasherati atengwe
1Yamkini habari imeenea ya kuwa miongoni mwenu kuna uzinzi ambao haujafanyika hata miongoni mwa watu wasiomjua Mungu: Kwamba mtu anaishi na mke wa baba yake. 2Nanyi mwajivuna! Je, haiwapasi kuhuzunika na kumtenga na ushirika wenu mtu huyo aliyefanya mambo hayo? 3Hata kama siko pamoja nanyi katika mwili, niko nanyi katika roho. Nami nimekwisha kumhukumu mtu huyo aliyetenda jambo hili, kama vile ningekuwepo. 4Mnapokutana katika Jina la Bwana wetu Isa nami nikiwepo pamoja nanyi katika roho, na uweza wa Bwana Isa ukiwepo, 5mkabidhini mtu huyu kwa Shetani, ili mwili wake uharibiwe, lakini roho yake iokolewe katika siku ya Mwenyezi Mungu.
6Majivuno yenu si mazuri. Je, hamjui kwamba chachu kidogo huchachusha donge zima la unga? 7Ondoeni chachu ya kale ili mpate kuwa donge jipya lisilotiwa chachu, kama vile mlivyo. Kwa maana Al-Masihi, Mwana-Kondoo wetu wa Pasaka#5:7 Sherehe iliyowakumbusha Waisraeli jinsi Mwenyezi Mungu alivyowakomboa kutoka utumwani huko Misri. amekwisha tolewa kuwa dhabihu. 8Kwa hiyo, tusiiadhimishe sikukuu hii kwa chachu ya zamani, chachu ya nia mbaya na uovu, bali kwa mkate usiotiwa chachu, ndio weupe wa moyo na kweli.
9Niliwaandikia katika waraka wangu kuwa msishirikiane na wazinzi. 10Sina maana kwamba msishirikiane na wazinzi wa ulimwengu huu, au wenye tamaa mbaya, wanyang’anyi au waabudu sanamu. Kwa kufanya hivyo ingewalazimu mtoke ulimwenguni humu. 11Lakini sasa nawaandikia kwamba msishirikiane na mtu yeyote anayejiita ndugu, hali akiwa ni mzinzi, au mwenye tamaa mbaya, mwabudu sanamu au msingiziaji, mlevi au mdhalimu. Mtu kama huyo hata msile naye.
12Yanihusu nini kuwahukumu wale watu walio nje ya kundi la waumini? Je, si mnapaswa kuwahukumu hao walio ndani? 13Mungu atawahukumu hao walio nje. “Ninyi mwondoeni huyo mtu mwovu miongoni mwenu.”#5:13 Kumbukumbu 17:7; 19:19; 21:21; 22:21, 24; 24:7

Iliyochaguliwa sasa

1 Wakorintho 5: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia