1 Yohana 1:8-10
1 Yohana 1:8-10 NENO
Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu. Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha kutokana na udhalimu wote. Tukisema hatujatenda dhambi, twamfanya yeye kuwa mwongo na neno lake halimo ndani yetu.