1 Yohana 2:3-6
1 Yohana 2:3-6 NENO
Basi katika hili twajua ya kuwa tumemjua, tukizishika amri zake. Mtu yeyote asemaye kuwa, “Ninamjua,” lakini hazishiki amri zake, ni mwongo, wala ndani ya mtu huyo hamna kweli. Lakini mtu yeyote anayelitii neno lake, upendo wa Mungu umekamilika ndani yake kweli kweli. Katika hili twajua kuwa tumo ndani yake: Yeyote anayesema anakaa ndani yake hana budi kuenenda kama Isa alivyoenenda.