Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Yohana Utangulizi

Utangulizi
Wasomi wa waraka huu walikumbwa na mafundisho hatari sana ya Wanostiki, waliofundisha kuwa kila kitu kilikuwa kiovu, isipokuwa roho pekee ndiyo nzuri. Kati ya mafundisho yao, walikana misingi ya imani ya wafuasi wa Al-Masihi, kama vile: hali ya Al-Masihi kuja katika mwili, mamlaka ya amri ya Al-Masihi, hali ya mwanadamu kuwa mwenye dhambi, na wokovu kuwa ni kazi ya Al-Masihi.
Mwandishi wa waraka huu aligundua ya kuwa jamii ya waumini ilikuwa katika hatari kubwa. Anawakumbusha waumini kuhusu umuhimu wa kuihifadhi imani, na kuwaeleza kuwa Al-Masihi alikuja katika mwili.
Mwandishi
Mtume Yohana.
Kusudi
Yohana anaonesha wazi kuwa Isa ni Mwenyezi Mungu aliyefanyika mwili, na hivyo kupinga kabisa ile dhana kwamba Al-Masihi aliwaziwa tu kama aliyekuwa na mwili, eti kwamba yeye alikuwa roho.
Mahali
Efeso.
Tarehe
Mnamo 85–90 B.K.
Wahusika Wakuu
Yohana na Isa.
Wazo Kuu
Si jambo gumu kupingana na mafundisho yanayokataa wazi misingi ya imani. Lakini mawazo potovu yanayofanana na kweli ya Injili yanapoingia, basi hili linakuwa tatizo kubwa.
Mambo Muhimu
Mwana wa Mwenyezi Mungu alikuja ulimwenguni katika mwili, alisikika na watu, alionekana, aligusika na walimkazia macho. Waraka huu unatangaza imani ya kweli katika Al-Masihi ni imani katika Mwenyezi Mungu kufanyika mwili, na maisha ya wafuasi wa Al-Masihi ni upendano wa ndugu.
Yaliyomo
Utangulizi (1:1-4)
Maisha ya mfuasi wa Al-Masihi (1:5–2:29)
Upendo wa kweli (3:1-24)
Imani na kuona kwa hakika (4:1–5:21).

Iliyochaguliwa sasa

1 Yohana Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia