Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Petro 1:10-12

1 Petro 1:10-12 NENO

Kwa habari ya wokovu huu, wale manabii waliosema kuhusu neema ambayo ingewafikia ninyi, walitafuta kwa bidii na kwa uangalifu mkubwa. Walijaribu kujua ni wakati upi na ni mazingira yapi ambayo Roho wa Al-Masihi, aliyekuwa ndani yao, alionesha alipotabiri mateso ya Al-Masihi na utukufu ambao ungefuata. Walifunuliwa kwamba walikuwa wanawahudumia ninyi, bali si wao wenyewe, waliponena kuhusu mambo hayo. Mmeambiwa mambo haya sasa na wale waliowahubiria Injili kwa Roho wa Mungu aliyetumwa kutoka mbinguni. Hata malaika wanatamani kuyafahamu mambo haya.