Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Timotheo 2

2
Maagizo kuhusu ibada
1Awali ya yote, nasihi kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote: 2kwa ajili ya wafalme na wale wote walio katika mamlaka, ili tupate kuishi kwa amani na utulivu, katika uchaji wote wa Mungu na utakatifu. 3Jambo hili ni jema, tena linapendeza machoni pa Mungu Mwokozi wetu, 4anayetaka watu wote waokolewe na wafikie kuijua kweli. 5Kwa maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani mwanadamu Al-Masihi Isa, 6aliyejitoa mwenyewe kuwa fidia kwa ajili ya wanadamu wote: jambo hili lilishuhudiwa kwa wakati wake ufaao. 7Nami kwa kusudi hili nimewekwa niwe mhubiri na mtume (nasema kweli katika Al-Masihi wala sisemi uongo), mwalimu wa watu wa Mataifa katika imani na kweli.
8Nataka kila mahali wanaume wasali wakiinua mikono mitakatifu pasipo hasira wala kugombana.
9Vivyo hivyo nataka wanawake wajipambe kwa adabu na kwa heshima katika mavazi yanayostahili, si kwa kusuka nywele, kuvalia dhahabu, lulu au mavazi ya gharama kubwa, 10bali kwa matendo mazuri kama iwapasavyo wanawake wanaokiri kuwa wanamcha Mungu.
11Mwanamke na ajifunze katika utulivu na utiifu wote. 12Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha au kuwa na mamlaka juu ya mwanaume. Mwanamke inampasa kukaa kimya. 13Kwa maana Adamu aliumbwa kwanza, kisha Hawa. 14Wala si Adamu aliyedanganywa, bali ni mwanamke aliyedanganywa akawa mkosaji. 15Lakini mwanamke ataokolewa kwa kuzaa kwake, wakiendelea kudumu katika imani, upendo na utakatifu, pamoja na kuwa na kiasi.

Iliyochaguliwa sasa

1 Timotheo 2: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia