Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Wafalme Utangulizi

Utangulizi
Kwa kuwa kitabu cha 1 Wafalme na hiki cha 2 Wafalme ni historia moja inayoendelea, taarifa za msingi za kitabu hiki cha 2 Wafalme ziko katika utangulizi wa 1 Wafalme.
Mwandishi
Mwandishi wa kitabu hiki hajulikani, lakini mapokeo ya Kiyahudi yanasema ni nabii Yeremia, au kikundi cha manabii.
Kusudi
Kuonesha yale yatakayowapata wale wanaokataa kumfanya Mwenyezi Mungu kuwa kiongozi wao wa kweli.
Mahali
Katika nchi ya Israeli.
Tarehe
Wakati kitabu hiki kiliandikwa haujulikani.
Wahusika Wakuu
Ilya, Al-Yasa, mwanamke Mshunami, Naamani, Yezebeli, Yehu, Yoashi, Hezekia, Senakeribu, Isaya, Manase, Yosia, Yehoyakimu, Sedekia, na Nebukadneza.
Wazo Kuu
Kuanguka kwa falme zote mbili za Israeli na Yuda kulisababishwa na kutokutii maagizo ya Mwenyezi Mungu, na kuishi maisha ya dhambi. Hali hii iliwapelekea kuwa mateka na kukaa utumwani, nayo miji yao ikaharibiwa; hii ilikuwa hukumu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Mambo Muhimu
Kitabu hiki kinaelezea kuhusu majanga mawili yaliyosababisha kuanguka kwa Israeli na Yuda. Janga la kwanza ni kuharibiwa kwa Samaria, mji mkuu wa Israeli, na taifa la Israeli kupelekwa utumwani. Janga la pili ni kuharibiwa kwa Yerusalemu, mji mkuu wa Yuda, na taifa la Yuda kupelekwa utumwani.
Yaliyomo
Ilya na Al-Yasa (1:1–8:15)
Wafalme wa Israeli na wa Yuda (8:16–17:6)
Israeli kutekwa kwenda Ashuru (17:6-41)
Wafalme wengine wa Yuda (18:1–24:20)
Kuanguka kwa Yerusalemu (25:1-30).

Iliyochaguliwa sasa

2 Wafalme Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha