Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Samweli 24:10-17

2 Samweli 24:10-17 NEN

Dhamiri ya Daudi ilishtuka baada ya kuwahesabu wapiganaji, naye akamwambia BWANA, “Nimefanya dhambi kubwa kwa kufanya jambo hili. Ee BWANA, sasa ninakusihi, ondoa hatia ya mtumishi wako. Nimefanya jambo la kipumbavu sana.” Kabla Daudi hajaamka kesho yake asubuhi, neno la BWANA lilikuwa limemjia Gadi nabii, aliyekuwa mwonaji wa Daudi, kusema: “Nenda ukamwambie Daudi, ‘Hivi ndivyo asemavyo BWANA: Ninakupa wewe uchaguzi wa mambo matatu. Nichagulie mojawapo nitakalotenda dhidi yako.’ ” Basi Gadi akaenda kwa Daudi na kumwambia, “Je, ije njaa ya miaka mitatu katika nchi yako? Au miezi mitatu ya kukimbia adui zako wakikufuatia? Au siku tatu za tauni katika nchi yako? Basi sasa, fikiri juu ya hilo na uamue jinsi nitakavyomjibu huyo aliyenituma.” Daudi akamjibu Gadi, “Nitataabika sana. Afadhali tuangukie mikononi mwa BWANA, kwa maana rehema zake ni kuu, lakini usiniache nianguke mikononi mwa wanadamu.” Basi BWANA akatuma tauni katika Israeli kuanzia asubuhi mpaka mwisho wa muda ulioamriwa, wakafa watu 70,000 kuanzia Dani hadi Beer-Sheba. Malaika aliponyoosha mkono wake ili kuangamiza Yerusalemu, BWANA akahuzunika kwa sababu ya maafa, akamwambia yule malaika aliyekuwa anawadhuru watu, “Yatosha! Rudisha mkono wako.” Wakati huo malaika wa BWANA alikuwa kwenye sakafu ya kupuria ya Arauna, Myebusi. Ikawa Daudi alipomwona huyo malaika aliyekuwa akiwaua watu, akamwambia BWANA, “Mimi ndiye niliyetenda dhambi na kukosa. Hawa ni kondoo tu. Wamefanya nini? Mkono wako uwe juu yangu na nyumba yangu.”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 2 Samweli 24:10-17