Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo 15:36-41

Matendo 15:36-41 NEN

Baada ya muda, Paulo akamwambia Barnaba, “Turudi tukawatembelee ndugu katika miji yote tuliyohubiri neno la Bwana tuone jinsi wanavyoendelea.” Barnaba alitaka wamchukue Yohana aitwaye Marko waende naye. Lakini Paulo aliona si vyema kwa sababu aliwahi kuwaacha walipokuwa huko Pamfilia, hakutaka kuendelea kufanya kazi naye. Pakatokea ubishi mkali kati ya Paulo na Barnaba kuhusu jambo hili, hivyo wakagawanyika. Barnaba akamchukua Yohana Marko wakasafiri baharini kwenda Kipro. Lakini Paulo akamchagua Sila na akaondoka baada ya ndugu kuwatakia neema ya Bwana. Akapitia Shamu na Kilikia, akiimarisha makanisa ya huko.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Matendo 15:36-41