Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo 15:36-41

Matendo 15:36-41 SRUV

Baada ya siku kadhaa Paulo akamwambia Barnaba, Haya! Turejee sasa tukawaangalie hao ndugu katika kila mji tulipolihubiri neno la Bwana, wako hali gani. Barnaba akaazimu kumchukua Yohana aliyeitwa Marko pamoja nao. Bali Paulo hakuona vema kumchukua huyo aliyewaacha huko Pamfilia, asiende nao kazini. Basi palitokea mashindano baina yao hata wakatengana. Barnaba akamchukua Marko akaabiri kwenda Kipro. Lakini Paulo akamchagua Sila, akaondoka, akiombewa na wale ndugu apewe neema ya Bwana. Akapita katika Shamu na Kilikia akiyaimarisha makanisa.

Soma Matendo 15

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Matendo 15:36-41