Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Amosi 2

2
1Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu:
“Kwa dhambi tatu za Moabu,
hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.
Kwa sababu alichoma mifupa ya mfalme wa Edomu,
ikawa kama chokaa.
2Nitatuma moto juu ya Moabu
ambao utateketeza ngome za Keriothi.
Moabu ataanguka kwa ghasia kubwa
katikati ya kelele za vita, na sauti ya tarumbeta.
3Nitamwangamiza mtawala wake
na kuwaua maafisa wake wote pamoja naye,”
asema Mwenyezi Mungu.
4Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu:
“Kwa dhambi tatu za Yuda,
hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.
Kwa sababu wameikataa Torati ya Mwenyezi Mungu
na hawakuzishika amri zake,
kwa sababu wamepotoshwa na miungu ya uongo,
miungu ambayo babu zao waliifuata.
5Nitatuma moto juu ya Yuda
ambao utateketeza ngome za Yerusalemu.”
Hukumu kwa Israeli
6Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu:
“Kwa dhambi tatu za Israeli,
hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.
Wanawauza wenye haki kwa fedha,
na maskini kwa jozi ya viatu.
7Wanakanyaga juu ya vichwa vya maskini,
kama vile juu ya mavumbi ya nchi,
na kukataa haki kwa waliodhulumiwa.
Baba na mwanawe hushiriki msichana mmoja,
kwa hivyo hulinajisi Jina langu takatifu.
8Watu hulala kando ya kila madhabahu
juu ya nguo zilizowekwa rehani.
Katika nyumba ya mungu wao hunywa mvinyo
ulionunuliwa kwa fedha walizotozwa watu.
9“Nilimwangamiza Mwamori mbele yao,
ingawa alikuwa mrefu kama mierezi,
na mwenye nguvu kama mialoni.
Niliyaangamiza matunda yake juu
na mizizi yake chini.
10“Niliwapandisha toka Misri,
na nikawaongoza miaka arobaini jangwani
niwape nchi ya Waamori.
11“Pia niliinua manabii kutoka miongoni mwa wana wenu
na Wanadhiri kutoka miongoni mwa vijana wenu.
Je, hii si kweli, enyi watu wa Israeli?”
asema Mwenyezi Mungu.
12“Lakini mliwafanya Wanadhiri kunywa mvinyo
na kuwaamuru manabii wasitoe unabii.
13“Sasa basi, nitawaponda
kama gari linavyoponda likiwa limejazwa nafaka.
14Mkimbiaji hodari hatanusurika,
wenye nguvu wataishiwa nguvu zao,
na shujaa hataweza kuokoa maisha yake.
15Mpiga upinde atakimbia,
askari wapiga mbio hawataweza kutoroka,
na mpanda farasi hataokoa maisha yake.
16Hata askari walio mashujaa sana
siku hiyo watakimbia uchi,”
asema Mwenyezi Mungu.

Iliyochaguliwa sasa

Amosi 2: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia