Wakolosai Utangulizi
Utangulizi
Nyaraka za Waefeso na Wakolosai zinaitwa pacha kwa sababu mambo yaliyomo yanafanana. Timotheo alishirikiana na Paulo huko Rumi katika kuandika nyaraka hizi mbili; Wakolosai ni mojawapo ya nyaraka za gerezani. Tikiko ndiye aliupeleka waraka huu Kolosai.
Mji wa Kolosai ulikuwa umejengwa kama kilomita 160 kutoka Efeso kwenye Bonde la Lika, karibu na Hierapoli na Laodikia. Kwa kadiri ionekanavyo, Paulo alikuwa hajautembelea mji wa Kolosai, ila mji huu ulihubiriwa Injili na Epafra wakati Paulo alikuwa Efeso. Paulo alipata kuwafahamu waumini hawa akiwa Efeso katika safari yake ya pili kueneza Injili. Sasa alikuwa na wasiwasi kwa sababu alisikia kuwa mafundisho ya Unostiki yalikuwa yameingia katika kundi hilo la waumini. Mafundisho haya yalikuwa yakiuelekeza ujumbe wa Injili hatarini.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Kusudi
Kupinga mafundisho ya uzushi katika kundi hilo la waumini, na kuwaonesha waumini kwamba wana kila kitu wanachokihitaji katika Al-Masihi.
Mahali
Rumi.
Tarehe
Mnamo 60 B.K.
Wahusika Wakuu
Paulo, Timotheo, Tikiko, Onesimo, Aristarko, Marko, na Epafra.
Wazo Kuu
Kuthibitisha utoshelevu wa Al-Masihi, ukilinganishwa na utupu wa filosofia ya mwanadamu.
Mambo Muhimu
Mambo yaliyokuwa yakiwasumbua Wakolosai: Mchanganyiko wa elimu ya nyota, uchawi, na mafundisho ya Unostiki ambayo yalisema kwamba Al-Masihi alikuwa sawa na malaika.
Yaliyomo
Salamu, shukrani na maombi (1:1-14)
Isa Al-Masihi na waumini (1:15–2:7)
Hatari za mafundisho ya uongo (2:8-23)
Mafundisho kuhusu maisha ya wafuasi wa Al-Masihi (3:1–4:1)
Maagizo zaidi, na mausia ya mwisho (4:2-18).
Iliyochaguliwa sasa
Wakolosai Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.