Danieli 2:20-22
Danieli 2:20-22 NEN
na akasema: “Lihimidiwe jina la Mungu milele na milele; hekima na uweza ni vyake. Yeye hubadili nyakati na majira; huwaweka wafalme na kuwaondoa. Huwapa hekima wenye hekima, na maarifa wenye ufahamu. Hufunua siri na mambo yaliyofichika; anajua yale yaliyo gizani, nayo nuru hukaa kwake.