Kutoka 39:42-43
Kutoka 39:42-43 NENO
Waisraeli walikuwa wamefanya kazi yote sawasawa na vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amemwagiza Musa. Musa akakagua kazi na kuona kuwa walikuwa wameifanya sawasawa na jinsi Mwenyezi Mungu alivyokuwa ameagiza. Kwa hiyo Musa akawabariki.